Pages

BOB JUNIOR VS SHOGA; JE NI KWELI BOB JUNIOUR NI SHOGA?

Raheem Nanji ‘Bob Junior’.
HATIMAYE staa wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ ameifungukia skendo yake ya kwamba yeye ni shoga,
Akizungumza kupitia kipindi cha runinga moja usiku wa Ijumaa iliyopita, Bob Junior alisema chanzo cha yeye kudaiwa ni shoga ni wimbo wake maarufu wa Oyoyo.

Alisema mara baada ya kuitoa video ya wimbo wake huo akiwa anakata sana mauno, watu walikuwa wakimpigia simu, wengine wakimtumia meseji kwamba, anaonekana ni ‘chakra’ maana anayaweza sana mauno.
“Watu wanasema mimi ni shoga, lakini si kweli. Kisa kilianzia kwenye ule wimbo wangu wa Oyoyo. Unajua katika video ya ule wimbo nilikata sana mauno, watu wakaamini mimi shoga.
“Wengine walikuwa wakinitumia hata meseji wakiamini hivyo. Kwa hiyo sababu kubwa ni ile video tu, watu wana mambo ya ajabu sana,”
alisema Bob Junior huku watu  alioongozana nao usiku huo wakitingisha vichwa kukubaliana naye.
Ishu ya Bob Junior kuonekana ni chakra pia iliwahi kusababisha amfikishe kortini kwenye Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akidaiwa kumtukana msanii huyo matusi ya nguoni likiwemo hilo la ushoga.
Katika kesi hiyo iliyofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa mara ya kwanza Mei 4, 2011 na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mariam Masamalo, Wema alihukumiwa kulipa faini ya shilingi 40,000 au kwenda jela miezi 6 ambapo alifanikiwa kulipa.

No comments:

Post a Comment