Pages

DIAMOND THE PLATNUM NA MASTAA WA KIKE MAARUFU! INASEMEKANA HAWA WASANII WA KIKE WALISHAWAHI KUWA NA UHUSIANO NA DIAOMOND HAYA CHECK CV YAKE HII!


AMA kweli ‘Diamond’ Nasibu Abdul ni sukari ya warembo! Nyota yake inazidi kung’aa kwa upande wa vimwana akidaiwa kuzidi
kuwaweka kwenye foleni ya Tuko Wangapi? Katikati ya mwaka huu, alishika rekodi ya kufikisha mademu 5 licha ya kuwa na umri wa
miaka 23, lakini mpaka Novemba hii amefunga 11, ongezeko ni 6, Amani linajua kila kitu!
 
Diamond akiwa na Najma.

  Wema Sepetu ambaye ni mpenzi wa milele wa Diamond, aligonga wanaume wake 5 ndiyo sababu ya kuwa NGOMA DROO.
Kwa Diamond idadi hiyo ya wasichana inatisha kutokana na umri wake huku umaarufu ukichangia kwa kiasi kikubwa kuwanasa
warembo hao wa mjini wanaopenda  ‘majina makubwa’.
...akiwa na Aunt Ezekiel.
Idadi ya 11 kwa ‘Mnyama’ huyo imetimia baada yakuzinasa picha akiwa na mwanamitindo maarufu Bongo, Nelly Kamwelu
huku wakidaiwa wawili hao kuna kitu ndani yake, hasa kinachohusu mahaba.

Madai hayo yanaongezwa nguvu na picha hizo ambazo zinawaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi mbalimbali ya kimahaba.
“Kwa sasa Diamond yuko juu sana, imefikia hatua anawapanga foleni mademu kwa sababu wengi wao wanataka kuwa na kijana
maarufu kama yeye,”
alisema mmoja wa waliozishuhudia picha hizo.
...akiwa na Nelly Kamwelu.
Baada ya kuzinyaka taarifa za Diamond kudaiwa kutoka na Nelly,Tulingia mzigoni na kufanya upembuzi yakinifu ambapo
ilibainika kuwa, ukiachilia mbali mrembo huyo, tayari Diamond alishadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mademu wengine
kibao.
UPENDO MUSHI
Maarufu kama Pendo wa Maisha Plus. Huyu alianza kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na  Diamond. Kuna wakati aliingia
kwenye bifu na Jacqueline Wolper akidai amemchukulia mpenzi wake huyo.
.
..akiwa na Wema Sepetu.
REHEMA FABIAN
Pia alitajwa kutoka kimapenzi na Diamond. Walipotafutwa kwa simu, Rehema alikiri lakini Diamond alichomoa akidai wanafahamiana tu.
JACQUELINE WOLPER
Kama ilivyoandikwa awali, alidaiwa kutoka na Diamond wakati hana jina kubwa kama alivyo sasa. Walipotafutwa wote, Diamond
alikanusha, Wolper pia aliruka kimanga, lakini watu wa karibu yao waliitaja hata hoteli waliyokuwa wakikutana, ipo Magomeni Kagera, Dar.
AUNT EZEKIEL
Huyu mdada ambaye sasa ni mke wa mtu, yeye aliwahi kudaiwa kulala na Diamond kwenye hoteli moja maarufu mitaa ya Bamaga,
Dar. Walipotafutwa, Aunt alikiri kuwepo kwenye hoteli hiyo akisema alikuwa na mpenzi wake ambaye ni rafiki wa Diamond.
Diamond pia alikiri kuwepo kwenye hoteli hiyo, lakini akasema alimfuata rafiki yake ambaye ndiye mpenzi wa Aunt! Mh!
...akiwa na Wolper.
NATASHA
Huyu mrembo ameshaonekana kwenye moja ya video za Diamond katika wimbo wa Moyo Wangu. Aliwahi kuingia kwenye bifu na Wema Sepetu akituhumiwa kutoka na msanii huyo wa Bongo Fleva. Mwenyewe alikiri kwa mapaparazi, lakini Diamond kama kawaida yake, akachomoa.
WEMA SEPETU
Amekuwa na Diamond kwa miaka miwili sasa ila mapenzi yao yako hivi; wanaachana, wanarudiana, wanaachana wanarudiana. Kifupi ni wapenzi hata sasa.
...akiwa na Jokate.
JOKATE MWEGELO
Huyu ndiye alidaiwa na Wema kwamba aliingilia penzi la ‘sukari wake’. Alimtuhumu kutoka na Diamond, ikawa uhasama mitaani  na
habari ya mjini kwa wakati huo ikawa Wema, Diamond na Jokate.
Jokate amekuwa akikana kutoka na Diamond japo ushahidi wa kimazingira upo, Diamond awali alikataa, kuna siku akakiri.
NUZLAH ABOUBAKAR
Katika ziara yake ya kimuziki Mombasa, Kenya, Diamond alikutana na huyu mrembo.  Picha za wawili hao wakiwa kwenye pozi la
kimahaba zikasambaa mtandaoni. Wakadaiwa ni wapenzi lakini Diamond akishindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu madai  hayo.
.
..akiwa na Nuzlah.
NAJMA
Huyu mrembo amesharipotiwa kama wenzake, kwamba anatoka na ‘Platnamz’, ilikuwa siri sasa si siri tena. Juzikati tu hapa, Diamond alichomoa kwenda kwenye ‘bethdei’ ya msichana huyo iliyofanyika Mbezi, Dar akisingizia alikuwa bize.

HUYU HAPA NELLY
Baada ya kujiridhisha kwa Diamond ‘kuwapitia’ mastaa hao 10, achilia mbali wale wa ‘mechi’ za mchangani, lilimtafuta Nelly ili  kumpa haki yake ya kujieleza kuhusu madai hayo, akafunguka:
“Haaaa! Jamani! Kweli kwa siku hizi nipo karibu sana na Diamond, kwa sababu namsaidia mambo kibao wakati akiandaa video ya wimbo wake mpya (Nataka  kulewa), nikawa napiga naye picha mbalimbali ambazo nilizipost BBM.
“Lakini hakuna sehemu yoyote niliyowahi kumtaja Diamond ni mpenzi wangu, ila nilijua watu watakuja kuzusha kuwa natoka naye ndiyo kama hivi sasa.
“Mimi nina mchumba wangu hata Diamond anamjua na nipo naye kwa zaidi ya miaka sita sasa ingawa hivi karibuni tulikuwa na matatizo ambayo tayari tumeshayamaliza. Diamond ni rafiki tu. Lakini kama ishu ipo kwenye kupiga picha, mbona akina Najma, Wema, Jokate wameshapiga picha na Diamond?”
Kwa upande wake Diamond, alipopatikana kwenye simu na kuulizwa kuhusu Nelly, alitoa sauti yenye maneno haya:“Nelly kwa sasa ni zaidi ya dada yangu maana kuna mambo kibao ananisaidia kwenye ‘shooting’ ya video ya wimbo wangu mpya, nilimuomba anisaidie kwa kuwa ana uzoefu wa mambo ya mitindo. “Sina uhusiano naye zaidi ya kazi na urafiki wa kawaida ambao mtu yeyote anaweza kuwa nao.”


JAMANI HUU NI MTAZAMO TU WEW JE UNASEMAJE?

No comments:

Post a Comment