Wiki kadhaa zilizopita mkali wa bongo flava hitmaker wa ngoma kama ‘Mdananda’, ‘Nimechokwa’ na ‘Nidanganye’, Shetta, alitangaza juu ya ujio wa ngoma yake mpya aliyopanga kumshirikisha msanii Lady Jay Dee.
Kupitia Power Jams ya East Africa Radio, Shetta ameelezea mabadiliko yaliyojitokeza juu ya wimbo huo ambao imebidi amshirikishe Linah na sio Jay Dee kama alivyotangaza awali. Amesema hapo awali alikuwa ameshawasiliana na Jide aliyemkubalia kufanya nae wimbo huo na kumpatia title ya wimbo ili aweze kujiandaa nayo. Mabadiliko yalikuja kujitokeza baada ya Jide kuiskia mistari ya Shetta ya wimbo huo kitu ambacho kilimsababisha kukataa kuimba katika wimbo huo kama walivyokuwa wamekubaliana mwanzo.
“Mwanzo alikuwa amekubali kabisa na nikampa title ya ‘Bonge la bwana’ lakini alipokuja kuiskia mistari akasema hakujua kama mimi nimeimba hicho nilichoimba so ni ngumu yeye kuimba sababu hafit kwenye idea hiyo maana hata kiumri yeye ni mkubwa kwangu, ila akasema labda niibadilishe kidogo idea kitu ambacho nimeona kitafanya na mimi nibadilike kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku ngoma tayari iko poa. So nimeamua kuifanya na Linah na Jide kasema poa nifanye na mtu mwingine halafu yeye ntakuja kufanya nae wimbo mwingine” alisema Shetta.
Shetta anategemea kuzindua ‘Bonge la Bwana’ pale New Maisha Club tarehe 25 mwezi huu wa November, na amewataja wasanii watakao mpa support katika show hiyo kuwa ni pamoja na Ferouz, Jaffarai, Pasha, One, Stereo, Young Dee, Shilole na wengine.
No comments:
Post a Comment