Pages

HIZI NDO SABABU ZA KUTOKWA NA UCHAFU NA HARUFU MBAYA KATIKA SEHEMU ZA SIRI



Kuna sababu nyingi ambazo
husababisha mwanamke
kutoa ute au majimaji

yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za

siri. Maambukizi ya bacteria

wanaosababisha magonjwa

kama Trichomoniasis,

Candidiasis, Gonorhear au

uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis

Bacteria n.k husababisha

mwanamke kutokwa na

uchafu unaoambatana na

harufu mbaya.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo

hazikutolewa wakati wa

hedhi huweza kusababisha

tatizo hili. Usafi wa sehemu

za siri usipozingatiwa

hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku

zake za hedhi, huweza

kuwa mazalia mazuri ya

bacteria wanaosababisha

harufu mbaya.


DALILI ZA UGONJWA WA VAGINOSIS

Mwanamke mwenye tatizo

la Vaginosis huwa na dalili

kubwa ya kutokwa na

ute na majimaji yasiyo ya

kawaida (Uchafu) kutoka sehemu za siri. Uchafu huu

huwa unatoa harufu kali

kama shombo ya samaki au

kitu kilichooza na

huambatana na maumivu

makali ya tumbo chini ya kitovu.

- Wakati mwingine uchafu

wenye rangi kama ya kijani

hutoka

- Kuwashwa na

kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa

tiba haraka husababisha

vidonda sehemu za siri.

- Mwanamke anapoona

anatokwa na ute

uliochanganyika na na damu hata kama hayupo

kwenye siku zake, hii ni

dalili nyingine ya Vaginosis.

- Maumivu makali wakati

wa tendo pia ni dalili za

ugonjwa huu.


MATIBABU

Tatizo hili hutibika

hospitalini baada ya vipimo

vya kitaalamu kuchukuliwa

na daktari au nesi mwenye

uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake.

Dawa za kupaka

(Ointment/ Cream) na dawa

za kumeza (Pills) huweza

kumaliza tatizo hili.


Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata

ushauri wa kitaalamu

kutoka kwa daktari au

nesi.

No comments:

Post a Comment