maisha yangu ya ndoa yalikuwa mazuri na matamu sana kipindi cha mwanzo, mapenzi yalikuwa tele na ya moto lakini ikafika kipindi mume wangu akabadilika akawa kituko akawa mlevi mapenzi hana yani tunaweza kukaa hata miezi mitano hatujakutana kimwili akija nyumbani siku nyengine anatafuta ugomvi tu ili tupigane, na mara nyengine hata haachi hela ya matumizi nyumbani...
kwa muda mrefu nikawa namvumilia nikidhani atabadilika lakini wala hata wazo alikuwa hana, siku moja nikiwa kwenye hotel moja na rafiki zangu akaja mkaka mmoja mtanashati na rafiki zake wakajumuika nasi, huyu mwanaume akatokea kunipenda na kwamatatizo niliyonayo sikuona mbaya kama ningekubali kupenda na kupendwa tena...
nikamuadithia kila kitu kuhusu ndoa yangu, na akaahidi kunipa mapenzi kama sijawahi kupewa penzi tena, kwakweli huyu kijana kama alikuwa ameshushwa kutoka Mbinguni alinipa mapenzi mpaka nikamuona mume wangu kama kaka yangu.....
miezi ikapita siku moja nikagundua yakwamba nimepitisha siku zangu za hedhi, kwenda kupima nikagundua ya kwamba ni mjamzito na kwasababu hatukutani kimwili na mume wangu nikajuwa moja kwa moja ni wa mpenzi wangu wa nje, kwakuwa sikuweza kumuacha mume wangu ikabidi siku hiyo nilivyorudi nyumbani nimtomase mume wangu mpaka akajikuta juu ya kifua changu, na ndipo ikawa mwanzo wa kulea ujauzito ule.....
baada ya wiki mbili nikamwambia mume wangu kwamba mimi ni mjamzito alifurahi sana kwasababu hatukuwa na mtoto basi kwake ilikuwa furaha kubwa, moyoni mwangu nikijuwa sio sahihi kutokumwambia baba halisi wa mtoto huyu kwamba nina ujauzito wake....
kwakweli baada ya kubeba mimba mume wangu akabadilika zile tabia zake mbaya zote zikafutika akawa na mapenzi tele, yani wakati ukafika mpaka nikawa nashindwa kwenda kuonana na mpenzi wangu wa nje, nikaachana naye bila kujuwa nilikuwa nimebeba mtoto wake...
sasa mimba ina miezi saba, mume wangu anajisifu kila mara kwa ndugu na rafiki zake anatarajia mtoto, moyoni roho inanisuta sijamtendea baba wa mtoto huyu haki lakini nitakapousema ukweli mume wangu ataumia sana na sitaeleweka na jamii pamoja na ndugu zake.....
najuwa sijafanya mema itafanyaje sasa ama niseme tu ukweli?

No comments:
Post a Comment