Muimbaji wa muziki wa Dansi Muumini Mwijuma 'Prince' ameikacha bendi ya African Stars 'Twanga pepeta' na kutimkia bendi ya Victoria Sound yenye makazi yake Mbagara, Dar es Salaam
Akizungumza jijini Dare es Salaam wakati wa utambulisho huo Mkurugenzi wa bendi hiyo ya Victoria Sound Daniel Mjema alisema kuwa wameamua kumuongeza muimbaji huyo kwenye bendi yao ili kuongeza nguvu na kuinua bendi hiyo iwe kama bendi nyingine
Alisema kuwa tumemchukua muimbaji huyu kwa mkataba wa miaka miwili na kazi kubwa atakayoifanya ni kuhakikisha anainua bendi bendi hii na kuifanya itambulike kama zilivyo nyingine kubwa, lakini pia kuwa na jukumu la kuchagua wanamuziki wakubwa wawili ili kujiunga na bendi hiyi
No comments:
Post a Comment