Mtayarishaji wa muziki P Funk Majani amefunguka kwa baadhi ya wasanii na wadau wa muziki kutothamini mchango wake katika muziki wa Bongo Fleva mpaka sasa ulipo fika
Hayo yalisemwa baada ya kupokea tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa Tanzania, tuzo ambazo ziliandaliwa na Baabkubwa Magazin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya muziki hususani Bongo Fleva
Alisema kuwa wasanii wengi wameingia katika muziki wa bongo fleva bila kutambua mchango wake katika muziki huo kitu ambacho hakileti heshima ya Bongo Fleva
"Bila mimi Bongo Fleva isingekuwepo ila watoto hawatambu mchango wangu wanadharau bila ya kujali nimeupigania vipi mziki huu mpaka kuufikisha hapa ulipo" alilalamika P Funk
Alisema kuwa mchango wake ni mkubwa katika muziki huo kutofautisha na thamani anayopeka katika tasnia hiyo pamoja na wadau wa muziki kiujula
Malalamiko hayo yametokana na kuwepo na muziki wa Bongo fleva nchini na watu kunufaika na muziki huo huku wakionekana kusahau mchango wa mtu aliyeibua mziki huo na kuufanya kuwepo ulipo sasa
No comments:
Post a Comment