Pages

UCHAWI NA USHIRIKINA UMETAWALA KWENYE JAMII ZA KIAFRICA ANGALIA PICHA ....MWANAMKE AKUTWA "AKIWANGA" CHUMBANI KWA MTOTO WA MIAKA TISA.


MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja (pichani) amepata aibu nzito baada ya kukutwa chumbani akidaiwa  kukiwangia kivulana, Hamis Abdallah ,9, maeneo ya Tegeta Kibaoni, Wilaya ya Kinondoni  jijini Dar es Salaam.

 Tukio hilo la aina yake lililopachikwa jina la ‘Aibu ya bi mkubwa

Ndani ya nyumba hiyo, mama huyo alikutwa akiwa amevaa nguo za ajabu na kufunga tunguri na shanga pamoja na vitu vingine vya ajabu  hali iliyotafsiriwa na wakazi wa eneo hilo kuwa ni vya kichawi na alikuwa anaenda kumwangia  mtoto huyo.

Akizungumza kwa masikitiko mtoto Hamisi alisema kwamba akiwa usingizini hakuweza kutambua mara moja kilichokuwa kikiendelea bali asikia kelele za majirani wakimwita  na kumwambia atoke ndani kwani alikuwa ameingia mchawi.

“Niliposikia kelele  hizo nilizinduka usingizini,  niliangaza macho  chumbani nikamuuona mwanamke wa ajabu akinichezea kama mtu anayechezea ngoma,” alisema Hamisi.!

No comments:

Post a Comment