Pages

Wimbo wa "Mama Kimwaga" wa Ngoma Africa band Wazua baraha ! Jimama Pesa lamsaka Kamanda Ras Makunja wa FFU ! kwa bakora mitaani !

the ngoma africa band press kit and logo 004.bmp

Bremen,Ujerumani.

Katika hali ya utatanishi kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta akipewa mashaka ya maisha na mwanamama moja kisa wimbo "Mama Kimwaga" ! ambao takribani mwezi mzima wimbo huo na nyingine za bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa mara na kituo cha Radio Funk haus,inayorusha matangazo mjini Bremen,Ujerumani. Mwanamama moja ambaye aliguswa sana na ujumbe wa nyimbo hiyo alihamua kutinga katika ukumbi wa mazoezi wa bendi hiyo mjini Oldenburg,mkononi akiwa na bakora ! mdomoni yakiwa yanamtoka maneno ya hasira,alisikika akidai kuonana na mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa aka FFU kamanda Ras Makunja,kwa bahati mbaya alijibiwa na wanamuziki walikua pale kuwa Kamanda hayupo,alipoulizwa kulikoni ?Jimama Pesa huyo alisikika akidai kuwa alikuja kumtia adabu Kamanda Ras makunja wa FFU,jimama pesa lilikoroma na kutema kibesi kuwa wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ujumbe wake unamnyima raha jimama huyo mwenye kuongea kiswahili kinachoonyesha kuwa anatoka nchi jirani kwa watani wa jadi. Jimama pesa hilo limedai kuwa akutegemea kabisa kama wimbo ule wa "Mama Kimwaga" ungepelekwa tena kwa maDJ wa redio Bremen na kurushwa hewani Ujerumani kote kwa kupitia sauti ya Funk Haus Europa, wanamuziki aka "maafande" wa Ngoma Africa band wakimtetea Boss yao Kamanda Ras Makunja,wamedai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa ma Dj wa redio kwa CD hiyo ilikuwapo pale redio siku nyingi,na katika CD hiyo aliyeimbwa ni "Mama Kimwaga"  sasa inakuaje ? kamanda asakwe
na bakora ka kushtumiwa kuwa anaziwia ridhiki ya mahitaji ya starehe ya jimama pesa .wanamuziki wa ngoma africa
wanamuhoji mwanamama anayemsaka kwa bakora kamanda wao Ras Makunja,ambaye mara nyingi anadaiwa kuwa ni mtunzi na mwimbaji mwenye darubini kali. wimbo huo pia unasikika at www.myspace.com/thengomaafrica pia
 at

No comments:

Post a Comment