Gari aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BNP lililopata ajali eneo la Tanangozi, Iringa lililokua likiendeshwa na Bw. Ezekiel Mwaiteleke (Marehemu) majira ya saa sita na nusu mchana na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo jana Desemba 4, mwaka huu.

Gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 840 BST likiwa na tela lake lenye namba T 566 BNQ likiwa limegongwa kwa nyuma na Toyota Rav 4 huko Tanangozi, Iringa na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja papo hapo.
Baadhi ya akina mama wasamaria wema wa Tanangozi, Iringa wakijaribu kumpepeleka mmoja ya majeruhi wa ajali iliyotokea jana eneo la Tanangozi, Iringa likihusisha Toyota Rav 4 T 770 BMP lililoingia nyuma ya tela lenye namba za usajili T 566 BNQ ambapo watu watano wa familia moja waliokuwa wakitokea Dar kwenda Mbeya walifariki papo hapo.
Na Francis Godwin, Iringa
AJALI mbaya imetokea mkoani Iringa jana mchana na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
AJALI mbaya imetokea mkoani Iringa jana mchana na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa -Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana.
Kwa mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Katika ajali hiyo abiria wote watano akiwemo baba na mama wa watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao walikufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Majina ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa gari hilo na baba wa familia hiyo, mkewe Grace Mwaiteleke, mtoto Kelvin Mwaiteleke (2), Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment