Pages

ANGALIA PICHA;WEMA ANASWA NA MWANAUME TATA

Wema akiwa na Anti Bilal Mashauz.

STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu amezua gumzo baada ya kunaswa akiwa katika  mikao ya ajabuajabu na mwanaume ‘tata’ maarufu kwa jina la Anti Bilal Mashauz.



Ishu hiyo ilipigwa chabo na paparazi wetu Alhamisi iliyopita kwenye viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar ambapo wawili hao walikwenda kusikiliza kesi ya msanii mwenzao, Kajala Masanja.
Wema na Anti Bilal, walinaswa viwanjani hapo wakirukiana ambapo Anti Bilal alionesha mapozi kama ya kike, kitendo ambacho kiliwakera baadhi ya Maustaadh waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi ya Shehe Ponda Issa Ponda.
Wawili hao walianza kujishebedua kwa kuchezeana ambapo Wema alionekana kushikana mashavu ya Anti Bilal ambaye alikuwa amemlegezea macho mrembo huyo.
“Mambo wanayofanya hapa siyo mahali pake, hivi hawaoni aibu kushikana vile mbele za watu?” alihoji mmoja wa mashuhuda.


No comments:

Post a Comment