Huenda Facebook ikafikia uamuzi wa kuichijia baharini Uganda katika orodha ya nchi inakopatikana kutokana na msimamo mkali wa nchi hiyo dhidi ya mashoga.
Hivi karibuni Uganda imejikuta kwenye kiti moto kutokana na msimamo wake kwa mashoga huku wabunge wakipanga kupitisha muswada wa sheria dhidi ya ushoga ambayo itakuwa na adhabu kali kwa jamii hiyo.
Hatua hiyo imezifanya baadhi ya nchi wahisani kutishia kuweka vikwazo vya kifedha na usafiri kwa viongozi walio mstari wa mbele kukandamiza haki za mashoga nchini Uganda.
Inadaiwa kuwa mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg atatoa tamko rasmi kuhusiana na Uganda.
Kama hatua hiyo ikichukuliwa makampuni mengi yanayotafuta kujijenga kupitia mtandao huo wa kijamii yataathirika vibaya.
WAMEANZA NA UGANDA...TUNAWASUBIRI WAJE NA TANZANIA ILI WAUONE MSIMAMO WETU.....
No comments:
Post a Comment