Pages

HAWA NDIO WAIGIZAJI 10 WA BONGO MOVIE WALIOFANYA VIZURI 2012


1. Jacob Stephen


Mwigizaji Jacob Stephen amekuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki baada ya kubeba uhusika kama inavyo takiwa na kufanya mashabiki wake kuvutiwa na kila kazi anayoitoa.
JB mwenye umri wa miaka 52 kwa sasa ana miliki kampuni yake ya Jerusalem Film Company ambayo inafanya vizuri baada ya kuzalisha filamu zaidi ya 23.
2. Steven Kanumba

Mungu amlaze mahali pema Steven Kanumba. Bado watanzania wanakubali kazi zake ambazo alizifanya kabla hajaiyaga dunia mwanzoni mwa mwaka huu.Katika tuzo zilizoandaliwa na jarida la Babkubwa, marehemu Kanumba alishinda tuzo ya muigizaji bora wa kiume.
3. Vincent Kigosi

Kama una kumbukumbu Vincent aka Ray na Kanumba ni watu waliokuwa wakishirikiana katika kazi zao na kuna kazi walizofanya pamoja. Ray The Greatest amekubalika na jamii kwa ubora wa filamu zake za mwaka jana ikiwemo Sister Marry.
Yeye na Brandina Chagula a.k.a Johari waliamua kujiunga na kuanzisha kampuni ya kuzalisha filamu iitwayo RJ Company.
4. Hisany Muya Tino

Katika soko la filamu Tino ni actor anayekuja kwa kasi kwenye filamu za mapigano ama action. Mwaka huu ametisha na filamu yake iitwayo CID.
Hapo awali Tino alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu nia yake ya kuachana na kuigiza filamu za mapenzi na kuamua kufanya za action ambazo ameonesha kuziweza.
5.Single Mtambalike

Pamoja na ukongwe, Single Mtambalike ameendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya filamu nchini. Kwa sasa ni mwandishi na muongozaji wa filamu. Pia ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya BULLS ENTERTAINMENT.
Waigizaji bora wa Kike wa mwaka 2012
1. Yvonne Cherryl Monalisa

Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ anaamini kuwa anastahili kuendelea kuwa mwigizaji bora wa kike katika tasnia ya filamu Tanzania, huku akiamini si kitu kinachopatikana kirahisi bali ni juhudi zake na kuwa makini kwa kile anachokifanya katika tasnia ya filamu.
Monalisa ni moja kati ya wasanii waasisi wa tasnia ya filamu hivi karibuni alitangazwa kama mwigizaji bora wa kike mwaka 2012 na jarida la Bab kubwa. Awali Monalisa amewahi kushinda tuzo nyingi zikiwemo za ZIFF.
2. Irene Uwoya
uwoya (600x800)
Muigizaji huyu mrembo bado ameendelea kuwa kipenzi cha wapenzi wengi wa filamu nchini kwa uwezo wake mkubwa wa kuigiza hasa kama msichana jeuri. Mwaka 2012 ameng’ara kwenye filamu kadhaa zikiwemo Dj Benny, Barmaid, Sister Marry na zingine.
3. Elizabeth Michael

Pamoja na kukabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia kutokana na kifo cha Kanumba mwaka huu. Elizabeth Michael aka Lulu bado ameendelea kung’ara katika filamu zilizotoka mwaka huu ikiwemo ile ya Woman of Principle aliyoigiza na Ray.
4.Wema Sepetu

Pamoja na kutoingia sokoni bado, Wema Sepetu mwaka 2012 alifanikiwa kufanya uzinduzi wa filamu uliotumia fedha nyingi zaidi kwa kumleta msanii mahiri Omotola Jalade kwenye uzinduzi wa Superstar.
Wema ameendelea kuonesha uwezo mkubwa kwenye filamu zingine alizoigiza zikiwemo Red Valentine, White Maria, Tafrani, Sakata, Crazy Tenant, Diary, Lerato na Dj Benny.
Mwaka 2012 alifanikiwa kufika kwenye fainali za Ijumaa Sexiest Girl ambapo mshindi alikuwa Jaqueline Wolper.
5.Jaqueline Wolper

Jacqueline Wolper Massawe mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl amekuwa kivutio kikubwa katika filamu kutokana na mvuto wake.
Filamu kama Taxi Driver, After Death,Malipo na Princess zilimng’arisha mwaka huu.
CREDIT KWA VITUKO VYA MTAA

No comments:

Post a Comment