kushuhudia onyesho la kwanza la Tamthilia mpya iitwayo Siri ya Mtungi. Tamthilia mpya hii ya
kusisimua itatangazwa kila wiki siku ya Jumampili saa 3:30 usiku kwa njia ya ITV na kurudiwa saa 3:30 usiku jumaatanu ifuatayo kwa njia ya EATV.
Tamthilia hii mypa imetekelezwa na JHU-CCP (John Hopkins Bloomberg School of Public
Health Center for Communication Programs); kwa msaada wa Watu wa Marekani (USAID – United States Agency for International Development) na PEPFAR (US President's Emergency
Fund for AIDS Relief). Ikiwa imetayarishwa na MFDI (Media for Development International) na
inwaleta pamoja Wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wana mitindo nguo,wakurugenzi wa
sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania. Pia tamthilia hii ni kati ya juhudi za programu ya awali ya TCCP (Tanzania Communication Capacity Project).
Katika maonyesho hayo, huko Msasani, wadau walikaribishwa na kupata fursah ya kuonana na waundaji, waandishi, waigizanji na watekelezaji wengine wa tamthilia hiyo. Pia walipata fursah ya kuhudhuria studio hiyo na kuona waigizaji wakiigiza kipande kidogo cha tamthilia hiyo pale pale studio akiwemo muigizaji mahiri hapa mjini wa Monalisa!
Kwa habari zaidi kuhusu Siri ya Mtungi jiunge na kurasa wao wa
Facebook (www.facebook.com/SiriyaMtungi) au fuatilia mtiriko wa uhondo huko Twitter kwa kujiunga na @SiriyaMtungi (http://www.twitter.com/SiriyaMtungi). Pia chukuwa fursah kupitia tovuti ya tamthilia (www.siriyamtungi.com
No comments:
Post a Comment