Pages

Jirani yangu anamtongoza mke wangu

 
SWALI-

Naitwa Ismail naishi Kijichi, Dar es Salaam, ndugu mshauri mimi nimepanga, kwenye hiyo nyumba kuna

kijana anayesoma Chuo Kikuu, huyu hajaoa. Siku za hivi karibuni amekuwa akimsumbua sana mke wangu kwa kumtaka kimapenzi. Mara zote amekuwa akimkatalia lakini jamaa hasikii anaendelea tu. Mimi sikuwa nafahamu hadi juzi baada ya mke wangu kuzidiwa ndipo aliponiambia ishu hiyo.

 Aisee kusema kweli roho iliniuma sana na ukizingatia huyo mvulana vitu vingi namsaidia mimi. Nimekuwa nawaza jinsi ya kumfanya ili akome tabia hiyo, lakini nashindwa, yaani huwa nashikwa na hasira kiasi cha kutamani hata kumuua. Mshauri naomba unishauri nifanyeje?

JIBU-

Kwanza ukiniambia mkeo kazidiwa na vishawishi vya huyo mvulana tayari natambua kuna unafiki fulani na pengine kuna taarifa potofu unazopewa. Mwanamke anayejiheshimu, mwenye msimamo na kujiamini, hawezi kusema amezidiwa nguvu na mwanaume anayemtongoza wakati yeye hamtaki kabisa.

Mara nyingi wanaume wanaopewa dalili za kukubaliwa ndiyo huwa ving’ang’anizi, lakini wanaokutana na wanawake jasiri wenye msimamo huwa hawawezi kurudia kauli za kutongoza mara ya pili.

Nakushauri kabla ya kumchukia huyo kijana mchukie mkeo kwa kuwa dhaifu na umwambie wewe au yeye hamna uwezo wa kumzuia mtu asimtongoze, lakini suala la kukubali au kukataa bado lipo mikononi mwake, asitake kukuchezea akili na kukugombanisha na watu kwa vitu ambavyo anaweza kuvikomesha hata bila ya kukuambia wewe!

No comments:

Post a Comment