Pages

MAMA KANUMBA AITWA NIGERIA

MAMA wa msanii wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Charles Kanumba, Flora Mtegoa amealikwa nchini Nigeria kwa ajili ya kupewa mkono wa pole kutokana na kifo cha mwanaye.

Akizungumza na paparazi wetu, mama Kanumba alisema ndani ya wiki hii ataondoka kuelekea Nigeria kwa siku kumi ili kupewa pole na mashabiki wa nchini humo.



“Nimepewa mwaliko na mashabiki wa Steven (Kanumba) kwa kuwa wao wameshindwa kuja huku kwa sababu ya gharama kubwa ukizingatia kuwa wako wengi,  hivyo wameona ni heri miye niende,” alisema.
Mashabiki hao wamemuahidi  mama Kanumba  kumzungusha sehemu zote muhimu nchini humo na kumlipia nauli ya kwenda na kurudi.
“Nimeshapata tiketi ya kwenda nchini humo, nadhani itakuwa ni fursa nzuri kwenda kuonana na mashabiki wa mwanangu,” alisema.
Enzi za uhai wake, Kanumba aliwahi kufanya ziara  nchini Nigeria na kumleta Bongo msanii maarufu wa nchi hiyo, Ramsey Noah na kucheza naye filamu ya Devil’s Kingdom.

No comments:

Post a Comment