Salome Ndumbangwe Misayo ‘Thea’.
IMEANDIKWA NA Hamida Hassan na Gladness Mallya
WAIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ na Salome Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ nusura wazichape baada ya Klabu ya Bongo Movie Unit kumgeuzia kibao mwanadada huyo kufuatia kitendo chake cha kuanika uozo unaofanywa na ‘memba’ wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, kisa cha wasanii hao kumgeuzia kibao Thea ni kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti ndugu la hili, Risasi Jumamosi iliyotolewa na mwanadada huyo ikilaani vitendo vinavyofanywa na waigizaji hao vinavyoichafua tasnia ya filamu kwa jumla.WAIGIZAJI Vincent Kigosi ‘Ray’ na Salome Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ nusura wazichape baada ya Klabu ya Bongo Movie Unit kumgeuzia kibao mwanadada huyo kufuatia kitendo chake cha kuanika uozo unaofanywa na ‘memba’ wa klabu hiyo.
Chanzo hicho kiliendelea kudadavua kuwa kasheshe lilitokea mara tu baada ya Thea na mumewe Michael Sangu ‘Mike’ kuingia kwenye pati ya mtoto wa msanii mwenzao, Shamsa Ford ambapo mwigizaji Mayasa Mrisho ‘Maya’ alimrukia kwa kumkaribisha huku akimsifia na kumkumbushia alichokisema gazetini kuwa ni kizuri kinaweza kusaidia watu kubadilika.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Maya alijifanya kumsifia sana Thea na kumwambia kuwa wasanii walikuja juu lakini yeye aliona ni sawa alichokisema ingawa kumbe alimsifia kwa unafiki kwani alipomuona Ray anatoka ndani akamgeuzia kibao na kuanza kuongea naye kwa kumgombeza,” kilisema chanzo.Hata hivyo, chanzo kiliendelea kudai kuwa Maya alipoona hajasikika akamuita Ray na kumwambia kama amemuona mbaya wao Thea?
Ilidaiwa kuwa baada ya kuambiwa hivyo, ndipo Ray akamdakia Thea na kuanza kumlaumu akimwambia hakutegemea kama angetoa siri za chumbani kwenye vyombo vya habari kwa sababu anamwamini kama dada yake.
Ilifahamika kuwa baadaye Ray alianza kupaza sauti akitaka kumkwida Thea ambaye naye alipandwa na hasira huku akimwelewesha kwa kutoa maelezo ili kumshusha waongee kwa ustaarabu.
Michael Sangu ‘Mike’.
Hata hivyo, Maya, baada ya kuona amezua timbwili aliondoka eneo hilo na kuwaachia ‘soo’ wenyewe ambapo kama siyo Mike na wasanii wenzake, Deogratius Shija, Nikita na Rado damu ingemwagika. Baada ya habari hiyo kujaa tele kwenye meza ya Ijumaa Wikienda, gazeti hili lilimtafuta Mike ambaye aliweka wazi kilichotokea na kudai kuwa Ray na Thea ni mtu na dada yake hivyo hawawezi kukwidana kwani mwisho walikaa na kuyamaliza.
No comments:
Post a Comment