Pages

ANGALIA PICHA :DAR LIVE NA SHAMRA ZA MWAKA MPYA, UZINDUZI ALBAMU YA ‘DOMO LA UDAKU’


 
Kundi la Kings Modern Taarab likikonga nyoyo za mashabiki kabla ya kuwapisha T Moto.
Umati ukirindima kwa burudani baada ya kutangaziwa kuwa mwaka mpya 2013 umeingia.
 
Kundi la T Moto likizindua albam yake ya ‘Domo la Udaku’.

Mkurugenzi wa T Moto, Amini Salmini (kushoto) na muimbaji wa kundi hilo, Jokha Kassim (aliyevalia shela kama bi harusi) wakiingia jukwaani kimadaha.
Wapambe walioshika shela kwa nyuma wakinogesha hafla hiyo.
 
Jokha akikamua.
Wacheza kiduku nao wakimrusha roho ‘bi harusi’ kwa pembeni.
 
Ukumbi mzima ukiwa na furaha ya kuuona mwaka mpya na burudani ya taarab.
Uzinduzi wa albam ukiendelea.
 
 Ni shangwe tupu ndani ya Dar Live.
 
‘Bi. Harusi’ akiondolewa jukwaani baada ya kumaliza kufanya makamuzi.
.Muimbaji mpya wa T Moto aliyetokea Kings Modern Taarab, Ustaadh Issa Ally, akikamua.
UMATI mkubwa wa wasaka burudani ulifurika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala katika kusherehekea mwaka mpya ambapo pia kundi la taarabu la T Moto lilizindua albam ya ‘Domo la Udaku’
                                      PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/ GPL 

No comments:

Post a Comment