Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) na wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni, wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na nusu asubuhi kufikisha malalamiko yao ya kutaka kupatiwa ulinzi katika Hosteli zao, zilizopo Kigamboni.
Wanafunzi hao wamefikia hatua hiyo, baada ya wenzao wawili wa kiume kubakwa na majambazi hadi kulazwa hospitalini, huku wakieleza kuwa kumekuwa na matukio kadhaa ya mara kwa mara ya kuvamiwa na majambazi na kulitaka jeshi la Polisi kutoa huduma ya ulinzi katika Hosteli zao.
Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili waweze kupatiwa ulinzi lakini hadi sasa ombi lao halijaweza kufanyiwa kazi na cha kushangaza zaidi ni kwamba, siku hiyo hiyo waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wa kiume walipovamiwa na kubakwa hali iliyosababisha wanafunzi kuzidi kuingia hofu ya kuishi katika Hosteli hizo.
Aidha wanafunzi hao wameeleza kuwa kila Majambazi hao wanapowavamia, wamekuwa wakiwataka wanafunzi hao vitu vya thamani kama Laptop, Simu za mkononi na fedha, ambapo kila mwanafunzi anayekaidi amri ya majambazi hao, humfanyia vitendo vya udhalilishaji kama kulawiti na mengineyo.
Wanafunzi hao wakiwa wamejazana katika kivuko cha Magogni, wakiteremka kivukoni kwa ajili ya kuelekea Wizara ya Mambo ya ndani. Pamoja na kutakiwa kupungua, wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho.
Wanafunzi hao wakiwa nje ya Jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani.
Askari wakilinda usalama.....
Kamanda Kova, akizungumza na wanafunzi hao pamoja na wanahabari wakati wa tukio hilo.
You might also like:
No comments:
Post a Comment