Ally Ramadhani 'Dogo Ally' akimtimulia vumbi mpinzani wake Theo John (hayupo pichani) wakati wa mashindano.
Ally Ramadhani 'Dogo Ally' akimtimulia vumbi mpinzani wake Theo John (hayupo pichani) wakati wa mashindano.
Dogo Ally akilia baada ya kushindwa kuendelea na mashindano.
ALLY RAMADHANI (16) aliyekuwa akishiriki mashindano ya pikipiki kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Morogoro aliangua kilio hadharani baada ya pikipiki yake kuharibika wakati akiongoza na hivyo kupitwa na mpinzani wake ambaye alishinda na kupewa zawadi.Theo John (30) ndiye aliyetangazwa mshindi wa shindano hilo japokuwa mashabiki wa Ally walitaka shindano hilo lirudiwe lakini watayarishaji walikataa.
Pamoja na kilio cha Ally, mashindano hayo yaliingia dosari wakati mmoja wa washiriki aliyejulikana kwa jina la George alipoanguka na kusababisha taharuki kubwa uwanjani hapo.
(PICHA/HABARI: DUSTAN SHEKIDELE, GPL / MOROGORO) & global publishers
No comments:
Post a Comment