Pages

VIDEO;KAMA HUJAWAH KUANGALIA SERIES YA SIRI YA MTUNGI ANGALIA HAPA!Onyesho la awali kwenye Siri Ya Mtungi - 5

Maisha yanazidi kumwendea ovyo Cheche pale anapoahidi kuwa mume mwema kwa kumsindikiza Cheusi kwenye kliniki ya uzazi. Wajibu wake kwa familia unaingia dosari hasa pale shangingi Lulu anapofika studio akitegemea zaidi toka kwa mpiga picha wake binafsi.
Stephen anakuwa hashikiki tena pale anaporudi na msichana kwenye banda la kaka yake, Duma.
Posa ya ndoa ya Mzee Kizito kwa Nusura ni ya dhati. Lakini Nusura bado hajaamua. Baba yake, Masharubu, anahakikisha kuwa Duma hawi kikwazo kwa muungano huu. Nusura anajikuta njia panda. Ni nini anachokitaka? Je anaweza kumwambia Duma kinachoendelea? Na nani atakayeyaangalia maslahi yake?

No comments:

Post a Comment