Leo hii kupitia 255 ya XXL, msanii anewakilisha Manzese, Ney wa Mitego, amethibitisha kumiliki gari lenye thamani ya sh milioni 35 aina ya Mark X.
"yaa ndio gari yangu mpya hiyo, nimenunua juzi kwenye show room ya jamaa mmoja hivi anaitwa Monea, kama milioni 35 hivi, mpaka ileee mi nakuwa nayo mkononi." amesema Nay
Kwa mziki anaofanya Nay, watu wengu wamejiuliza kama kweli mziki ndio ulimfanya kumiliki gari hilo ama kuna ishu zingine zimemuwezesha kupata ndinga hiyo."Mziki unachangia kwa asilimia kadhaa pia, ijapokuwa siwezi nikasema moja kwa moja ni mziki, lakini mziki umechangia, kuna hela ya mziki pia katika hili, mi ni mfanya biashara, nafanya biashara nyingi, aaah na mziki pia ni moja kati ya biashara zangu, so mziki pamoja na biashara zingine zinafanya mi naendesha maisha yangu, na nna miliki hivi ninayomiliki" amesema Nay
Ney pia amezungumzia kuhusu picha ambayo inaonekana kwenye mtandao wa facebook, inayomuonyesha akiwa hana shati, na akiwa ameshikilia bastola..
"Aaaah,mi nahisi siko tayari kulizungumzia hilo, siko tayari tu kuongelea chochote kuhusu hiki ambacho unaniuliza sasa hivi, lakini aaah nitakapo kuwa tayari nitasema nipo tayari na nitaongea kile ambacho ntaweza kukiongea." amesema Nay
No comments:
Post a Comment