Pages

SOMO LA LEO ( Kufanya Mapenzi Kipindi Cha Ujauzito )


 Habari zenu wapenzi wasomaji wangu! Katika mfululizo wa kusasambua leo naomba niongelee kuhusu kufanya mapenzi kipindi cha ujauzito! Nimefikia hatua mara baada ya mabishano na mijadala kadhaa ya watu wazima kuhusu mapenzi, staili na madhara kipindi cha ujauzito! kwa leo mimi ntasema machache nnaimani mengi yanajulikana tayari.
                  Kabla yote ieleweke kwamba wapo baadhi ya wanawake ambao inapofika kipindi cha Ujauzito huwa hawapendi hata kuguswa bega na waume zao, kama hali ikiwa hivi, mume usimmaind sana, elewa ni mapito tu na "atarudi kundini soon" Pia wapo baadhi ya wanawake ambao wanapokuwa na ujauzito basi hamu ya kufanya mapenzi huongezeka maradufu na inawezekana wakataka "Uroda" Kila siku, hapo pia mzee mwezangu jua ni mapito, yataisha tuu! Kikubwa ni kuelewa Mkeo yupo katika hali gani na kujitahidi kadri ya uwezo wako kwenda nayo sawa.
              Mbali na hayo napenda niseme kuwa "INAWEZAEKANA" kabisa Mume na Mke Kufanya mapenzi kipindi cha Ujauzito wa Mke mpaka siku anayojifungua, bila kuhofia eti utamjeruhi mtoto maana kabla haujafikia alipo mtoto kuna Matabaka ambayo yanamkinga mtoto na uvamizi wa nje hasa wa "Dudu" ya Baba!
Kuhusu Staili nakuomba mume usiwe unampinda sana Mkeo maana utakuwa unamuumiza tumbo, piga zile za kale tu! Pia Kama Mke unawasiwasi na Hali yako ni vizuri ukamwona Daktari wako wa Kliniki kwa maelezo au vipimo vya ziada!

NA MWANDISHI WA SASAMBUA THNX

No comments:

Post a Comment