Taarifa rasmi kutoka kwa klabu ya Everton zinasema kocha David Moyes ataondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
"Kocha alikutana na mwenyekiti Bill Kenwright mapema jana jioni na kumwambia matamanio yake ya kujiunga na Manchester United.
"Mwenyekiti, kwa niaba ya klabu, angependa kutoa shukrani za dhati kwa David kwa mchango wake mkubwa alioutoa tangu alipojiunga nasi March 2002. Amekuwa meneja wa wa aina yake."
Wakati huo huo Manchester United bado haijathibitisha kwamba Moyes ndio kocha atakayemrithi Sir Alex Ferguson
No comments:
Post a Comment