Iryn Namubiru, mwanamuziki kutoka nchini Uganda ambaye ameripotiwa kukamwatwa huko nchini Japan kutokana na tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya.
Ripoti zinaweka wazi kuwa, Iryn alienda nchini humo kwaajili ya kufanya show Jumamosi iliyopita, Tarehe 4 huko Tokyo, Yotsukaido Cultural Hall, na hadi dakika ya mwisho ya mpango huu, promota aliingia mitini, issue iliyomlazimu Iryn kuripoti tukio hili polisi.Story kwa mtaa ni kwamba kabla ya ziara hii, Iryn alikuwa apae kuelekea Japan sambamba na Dr Hilderman pamoja na King Michael lakini hawa wengine walichomoa hasa baada ya promota huyu aliyetambulika kwa jina la Kim Ueno kushindwa kuwalipa kiasi walichokubaliana kama advance kwaajili ya show na kwaajili ya ticketi zao za ndege kurudi Uganda.
VIA BAABKUBWA
No comments:
Post a Comment