Nafahamu kuwa kila mtu anayo namna yake ya kupika, ila recipe ninazo toa humu ni namna vile ninavyo pika mimi na huwa kinatoka kitamu tu na walaji wana enjoy
Jinsi ya kupika pilau la kuku/ au nyama nyingine yoyote unayoipenda wewe.
Ila kama ni la kuku atapendeza zaidi akiwa ni kuku wa kienyeji.
Ukishamkata kuku/nyama ukaosha vizuri, unaweka chumvi na ndimu.
Unabandika jikoni viive bila kuongeza maji, ikishakauka maji maji yote unakaanga mpaka iwe brown, au kama hupendi wa kukauka sana unakaanga kidogo tu
Halafu unahifadhi sehemu unasubiri ijichuje mafuta
Kumbuka pia kukaanga na viazi mbatata navyo uvihifadhi pembeni
Unaosha mchele unachuja maji yote kisha unauhifadhi kwenye chombo kikavu.
Pembeni unakuwa umekata kata viungo, Chumvi, Vitunguu, Nyanya ya ku blend, Karot ndogo ndogo ikibidi zikate kwa mshine sio kwa mkono,
Garlic ya kutosha pia uwe ume blend au wengine hupenda kuponda kwenye kinu kwa imani kuwa haitapoteza ladha yake ya asilia.
Mimi pia napenda kutwanga kwenye kinu badala ya kutumia blender.
Viungo vya Pilau vilivyo changanywa kwa pamoja, mdala sini (vile vimbao mbao)
Chemsha maji ya moto kwenye sufuria tofauti na utakalopikia pilau yako.
Baada ya kuwa umesha andaa vitu vyote hivyo unaanza kama ifuatavyo
Weka mafuta kwenye sufuria mpaka yachemke kabisa
Weka vitunguu, kaanga kidogo kisha ongeza karot. Acha vichemkie halafu ongeza nyanya ya kusagwa.
Funikia tena vichemke kidogo halafu weka vitunguu thaumu vilivyo sagwa, Ongezea na viungo vya pilau halafu acha tena kidogo.
Ukiona vimechanganyika vema, weka mchele, chumvi pamoja na maji kidogo.
Maji lazima yawe ya moto, jitahidi kuangalia kipimo cha maji kisizidi usije kutoa bokoboko.
Funikia huku ukiwa umepunguza moto ili kisiungue kwa chini.
Baada ya dakika kama 20 pilau lako litakuwa limewiva.
Unatayarisha chombo kikubwa unamwaga ule wali wote kisha unachanganya na Kuku/nyama pamoja na vile viazi ulivokuwa umevikaanga mwanzo. unafunika kwa dakika kama 5-10 ili mvuke wa harufu ya viungo uchanganyike na kuku/nyama na viazi.
Baada ya hapo unaweza kupakua na kuweka mezani na itakuwa tayari kwa kuliwa.
Usisahau kachumbari ya kiswahili kwa pembeni, ya Nyanya, Vitunguu na Matango au Chachandu
No comments:
Post a Comment