Pages

UDAKU KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS AIBU: MWANAUME AFUMANIWA NA MKE WA MTU GESTI AKIWA UCHI WA MNYAMA


Habari kamili zilizonaswa  na  waandishi  wetu  ni kwamba mwanaume aliyetajwa kwa jina la Baba Asha alidai kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba Tony akiwa gesti na mkewe (jina linahifadhiwa), tayari kwa kuvunja naye amri ya sita. 

Tukio hilo la aibu ya milenia lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya Pumzika iliyopo maeneo ya Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada ya kumtia mikononi ‘mwizi’ wake ambaye mbali na urafiki pia ni majirani, ndipo akamchakaza sura vibaya na kumsababishia kuvuja damu.
Habari za kina zilidai kuwa mke wa Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara ukaingia ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe akachukua kilongalonga hicho na kuufungua ujumbe huo.


Ilidaiwa kuwa mume alitaharuki kukutana na ujumbe uliokuwa ukimtaka mkewe kwenda Pumzika Guest House kukutana na jamaa huyo.

Iliendelea kudaiwa kuwa Baba Asha hakuyaamini macho yake, akausoma tena ule ujumbe na ndipo akagundua sms nyingine nyingi, vocha na fedha za mtandao alizokuwa akitumiwa mke wake kutoka kwa Baba Tony.

Chanzo kilidadavua kuwa baada ya kugundua mchezo mzima, Baba Asha akatulia na kumsubiri mkewe atoke bafuni ili kuliweka sawa suala hilo.

Ilifahamika kuwa mke aliporudi kutoka kuoga, mume hakuonesha dalili zozote, alichokifanya ni kumwita mkewe na kumwambia kuwa achague moja, kufungasha kilicho chake, aondoke nyumbani kwake au amwekee jamaa mtego anaswe ili ajue mke wa mtu ni sumu.

Jibu lilikuwa rahisi kwani alikubali kuweka mtego ili amnase mbaya wake ndipo atamsamehe.


Ilifahamika kuwa ilipita wiki moja kimyakimya kwani mara ya kwanza Baba Tony alichezwa na machale, alipofika kwenye gesti hiyo na kumwona mtu anayemfahamu, alimwambia yule mwanamke waahirishe.

Habari za uhakika ni kwamba wiki iliyopita, Baba Tony aliingia kwenye kumi nane, akajaa mzimamzima kwenye mtego wa fumanizi uliowekwa na Baba Asha na mkewe.


Mara baada ya kuona mwanaume mmoja (Baba Asha) akiwa na askari kwenye gesti hiyo akihaha, king’ora kililia kwenye akili ya mwandishi wetu ambaye hakufanya makosa, akamfuata mfumaniaji kwa nyuma hadi aliporuhusiwa kumfuata mkewe chumbani.



Chumbani mtiti ulikuwa mkubwa ambapo Baba Tony alikutwa kama alivyozaliwa huku mke wa mtu akiwa bado hajavua na ndipo mtiti ukaanza.

 Katika purukushani, Baba Asha alimpa kibano ‘mwizi’ wake hadi akamchana usoni na kumng’oa meno ya mbele, jambo lililosababisha kutokwa na damu nyingi.




Kama hiyo haitoshi, ili kuthibitisha kuwa mke wa mtu ni sumu, Baba Asha alimchoma jamaa huyo bisibisi kwenye makalio hadi askari alipoingilia kati na kumchukua mtuhumiwa kisha akamtoa nje.

Wakiwa nje ya gesti hiyo, Baba Tony aliomba kujisafisha damu na baada ya hapo alipigwa pingu tayari kwa kupelekwa Kituo cha Polisi, Pangani, Ilala...

SOURCE ; GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment