Pages

WORLD WONDERS; ANGALIA PICHA MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI NA MAPACHA WALIOVUNJA REKODI YA KUWA NA UMRI MKUBWA


Katika picha ni:Chandra Bahadur Dangi,raia wa Nepal akipewa Cheti na Mhariri Mkuu anayeshughulikia na kuhusika na watu waliovunja rekodi katika dunia hii katika mambo mbali mbali-Chief of Guinness World Records-bwana Craig Glanday.

Mheshimiwa huyu ,bwana Shortest man in the world, alipokea cheti hicho baada ya kutangazwa kuwa ndiye mwanaume mfupi zaidi wa kipekee anayeishi duniani kwa sasa na kwamba yeye ndiye mwanaume mfupi zaidi kuliko wanaume wote, aliyebahatika kuingia na kukitikisa kitabu cha record ya dunia.

Hii ilikuwa katika sherehe zilizofanyika mjini Katmandu,nchini Nepal,siku ya Jumapili tarehe 26,2,20012.

Hapo kama anavyoonekana katika picha si kwamba kakaa bali ndio kasimama hapo!.
Mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 72, baada ya kupimwa urefu,vipimo vilitapika majibu kuwa ana inchi 21.5,(sawa na sentimeta 54.6 kwa urefu).

Vipimo hivyo ndivyo vilivyompatia nafasi hiyo ya kuwa mwanaume wa kwanza mfupi kuliko wote aliyevunjua rekodi ya dunia,hivyo kumfanya ajinyakulie ile Title (au cheo) iliyokuwa inamilikiwa na mwanaume mwingine mfupi kupindukia,aliye itwa:

Junrey Balawing wa Ufilipino,ambaye yeye alikuwa na inchi 23.5,(sawa na sentimeta 60 kwa urefu).

Mapacha  Ena na Lily wametangazwa kuwa na umri mkubwa duniani, baada ya kusheherekea pamoja siku yao ya kuzaliwa ya 102. 



 
Mapacha hawa wametimiza miaka 102 na kupitishwa kuwa ni mapacha waliovunja rekodi ya dunia kwa pamoja.

Ena Pugh na Lily Millward, ambao walizaliwa tarehe 4 Januari 1910, wamekuwa wakishirikiana katika kusherehekea siku yao muhimu ya kuzaliwa, japokuwa mmoja wa mapacha hawa "Lily" kwa hivi karibuni alilazwa kwa matatizo ya nyonga lakini binti yake "Dianne Powell, 65, amedai kuwa mama yake  anaendelea vizuri huko hospitarini, japokuwa siku ya sikukuu yao pacha wake "Ena alimtembelea mwenzake hospitari na kula baadhi ya vipande vya keki pamoja.

Hata hivyo kikongwe Lily alitoboa siri yao ya kuishi miaka mingi duniani, " siri yetu  ya kuishi maisha marefu ni tumekuwa tukicheka au kufurahi na kutaniana sana.Tumekuwa tukifanya kazi shambani wakati mwingi, lakini tumekuwa tukifurahi kwa pamoja na tumekuwa na bahati ya kuwa ni watu wenye afya." alisema Lily.

Kwahiyo mpendwa msomaji unashauriwa japo kupunguza hasira na kuongeza furaha au kicheko katika muda wako.

No comments:

Post a Comment