STAA mkubwa wa filamu za Kibongo, Mahsein Awadh ’Dk. Cheni’, amevamiwa
na watu wawili wanaodaiwa ni vibaka na kufanyiwa fujo, kisa kikidaiwa
kuwa ni dhamana aliyomwekea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika
ile kesi ya kifo cha Steven Kanumba.
|
Steven Kanumba enzi za uhai wake.
DK CHENI ALIRIPOTI POLISI?
Amani lilipomuuliza ‘sosi’ huyo kama Dk. Cheni alikwenda kuripoti polisi, jibu la swali hilo lilikuwa ni hapana, sababu ikiwa ni mtendwa kushindwa kukariri namba za pikipiki. “Alishauriwa aende polisi lakini akasema hawezi kufanya hivyo kwa sababu wahusika hawafahamu na kwamba hana ushahidi wowote wa kuwafanya watuhumiwa wakamatwe HUYU HAPA DK. CHENI Baada ya kupata taarifa hizo, Amani lilimsaka Dk. Cheni ambaye alikiri kuvamiwa na watu hao na kupasua kioo cha gari lake lakini hawakumjeruhi. “Kumekuwa na matukio mengi ya ajabuajabu yananitokea, nadhani hivi sasa nitakuwa makini sana, nitaripoti polisi kila kitu, siwezi kuendelea kupuuzia,” Dk Cheni alisema. TUJIKUMBUSHE Dk. Cheni alijitahidi kwa hali na mali kumsaidia Lulu kutoka gerezani Segerea akikabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia katika kifo cha Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka jana ambapo alisota kwa muda wa takribani miezi kumi hadi alipotolewa kwa dhamana ya shilingi milioni 20, mwezi Machi mwaka huu. Hivi karibuni Dk. Cheni alilazwa katika Hospitali ya Buruhani iliyopo maeneo ya Posta, Dar, baada ya kula chakula kilichosadikiwa kuwa na sumu. Matukio hayo yanazidi kuibua maswali mengi na akitakiwa kuwa makini zaidi. |
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
UHUSIANO WA DK. CHENI, LULUTakribani miaka kumi iliyopita, Dk. Cheni alimfuata mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila akamuomba amwingize mwanaye kwenye sanaa ya uigizaji katika Kundi la Kaole. Dk. Cheni aliwahi kukiri kuwa mama Lulu alimkabidhi mwanaye awe baba mlezi katika sanaa, kazi ambayo staa huyo aliifanya. Hivyo kitendo cha kuwa ‘beneti’ na Lulu alipopata matatizo kilikuwa ni mwendelezo wa malezi anayompatia hadi sasa. KWA NINI LULU AMPONZE DK. CHENI? Swali linalokosa jibu ni hili la kwa nini Lulu amponze Dk. Cheni wakati huu akiwa uraiani ambapo baadhi ya wadau wa sanaa wamechangia mawazo kwa kusema huenda ni wivu wa kimapenzi au roho mbaya. “Unajua watu wengi wanataka kufanya kazi na Lulu, sasa wanapoona wanashindwa kumpata wanadhani Dk. Cheni anawabania. “Lakini pia inawezekana watu wanapomuona Dk. Cheni na Lulu wako pamoja wanadhani ni wapenzi, sasa kama Lulu alikuwa na mpenzi ni rahisi kuhisi amepinduliwa,” alisema Jenista Aron msanii chipukizi mkazi wa Kinondoni, Dar. |
No comments:
Post a Comment