G-Nako: Nako 2 Nako bado iko hai - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » G-Nako: Nako 2 Nako bado iko hai

G-Nako: Nako 2 Nako bado iko hai


Hivi karibuni mashabiki wengi wa kundi la Nako 2 Nako Soldiers la Arusha wamekuwa wakishindwa kuelewa kama kundi hilo limekufa kutokana na members wake kuwa karibu zaidi na kundi la Weusi.
Akijibu swali la Bongo5 kama Nako 2 Nako imeuliwa na Weusi, G-Nako amesema kundi hilo bado lipo na Weusi si kundi bali ni kampuni ambayo inajumuisha members watano ambao ni yeye, Lord Eyez, Nikki wa Pili, Joh Makini na Bonta.
“Chama lipo kama kawaida na soon kinaweza kikanuka kwasababu imeonekana kuwa kuna mkanganyiko Weusi, Nako 2 Nako, River Camp lakini soon tutaliclear hili na soon nyimbo ya Nako 2 Nako nafikiri nayo itatoka, alisema G Warawara.
Aliongeza kuwa walipokuwa pamoja kama Nako 2 Nako walishauriana kuwa kila mmoja anaweza kufanya kazi yake binafsi nje ya kundi.
Nako 2 Nako Soldiers inaundwa na Lord Eyez, G-Nako na Bou Nako. Ibra Da Hustler aliyekuwa mmoja wa member wa kundi hilo alijitoa.
Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template