Sharo Milionea Afunguka "Usharobaro Mgumu Sana Jamani" - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » Sharo Milionea Afunguka "Usharobaro Mgumu Sana Jamani"

Sharo Milionea Afunguka "Usharobaro Mgumu Sana Jamani"


KOMEDIAN aliyejitosa katika muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefunguka kuwa hakuna kitu kigumu kama kuishi kisharobaro kwani kunahitaji gharama kubwa.

Akizungumza na ‘kachala’ wa Wikienda Staa Shopping aliponaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo katika duka la Robby One lililopo Kinondoni jijini alisema ili uwe sharobaro wa ukweli inabidi usiwe mbahili katika kununua nguo kila mara ili uendane na staili hiyo ya usharobaro.
“Kweli kabisa ndugu yangu hutakiwi kuwa mbahili kwani ukiwa na tabia hiyo wavimba macho mitaani watakutungia jina la sharobaro mchafu,” alisema Sharo Milionea.
Komedian huyo alifanya shopping ya kununua vitu dukani hapo iliyogharimu kiasi cha shilingi laki mbili na ushee.
Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template