PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa uarabuni.
Wolper amesema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka tena kuwa na mpenzi wa Kibongo.
“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’.
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !