DIAMOND THE PLATNUM; SHOW YA DIAMOND PLATNUM @ NEW MAISHA CLUB NI VURUGU TUPU NA CHUPA KUTAWALA KWENYE UKUMBI! - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » DIAMOND THE PLATNUM; SHOW YA DIAMOND PLATNUM @ NEW MAISHA CLUB NI VURUGU TUPU NA CHUPA KUTAWALA KWENYE UKUMBI!

DIAMOND THE PLATNUM; SHOW YA DIAMOND PLATNUM @ NEW MAISHA CLUB NI VURUGU TUPU NA CHUPA KUTAWALA KWENYE UKUMBI!


Watu Wakiingia Maisha Jana
Jana Usiku ndani ya maisha club palikuwa na show kubwa ya Usiku Wa Wasafi ila haikwenda kama ilivyo pangwa na msafi Diamond.Watu waliingia club hio mapema na tayari kwa show kali kutoka kwa Diamond. Show ilianza saa saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo zilianza, Kundi kubwa la vijana wasiojulikana walianzan kutukana watu, kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa mashabiki wa Diamond. Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi Bestizo Mkononi.Bestizo ni Camera Men na Social Media Personal Wa Diamond kupitia Thisisdiamond.com. Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.


Chid Benz aliongea na watu na kusema sio kitu kizuri kufanya fujo kwenye onyesho la msanii kama Diamond.Kwani kama una chuki na Diamond mfate mtaani na sio kwenye show yake kwani unaweza kuleta matatizo kwa mashabiki wasio na hatia. Pia Chid Benz alimtuliza Diamond na kumuomba apande kwenye stage kumaliza show na kuburudisha fans waliolipa na kuja kumuona mtu wao. 


Vitu vya thamani kama Cheni,Pete na Camera ya Bestizo ya ThisisDiamond iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na Uongozi wa maisha ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio sababu ya show ya Diamond Kuharibika.

Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template