SAKATA LA WAVULANA WALIOOTA MATITI NA JINSI JAMII ILIVYOWATENGA - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » SAKATA LA WAVULANA WALIOOTA MATITI NA JINSI JAMII ILIVYOWATENGA

SAKATA LA WAVULANA WALIOOTA MATITI NA JINSI JAMII ILIVYOWATENGA



VIJANA watatu wa familia moja ya  Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.

Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni  Yeuri (17 ), Gabriel (11) na  Daniu Ramírez  (12),  hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo. 
Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao.
Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya  Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta  Pedro Antonio Delgado aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.”
Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template