Mbele ya steji ilikuwa imepambwa na cover za magazeti ya Baabkubwa yaliyopita na kusomwa na wengi.
Baghdady kwa steji akifanya vitu vyake
Huku burudani ikiendelea wengine walikuwa wakijisomea gazeti la Baabkubwa kama kawaida kabisa
Sam wa Ukweli alikuwa anatambulisha wimbo wake mpya pamoja na video yake mpya
Nadiriki kusema Club Maisha ilikuwa imejaa watu na joto lake lilikuwa si mchezo, kweli watu wanapenda uzalendo wa club yao, hata kuwe vipi lazima mtu asimame mwanzo mwisho atizame burudani
Kila siku iendayo kwa mungu napotizama show za DYNA napata picha nyingine mpya machoni mwangu kwa jinsi atakavyokuwa msanii wa kike anayetoa burudani kali kwa steji kwa maana anajipanga sana, BIG UP mdogo wangu
Baba Jonii akiwa kwa steji akimtambulisha Gadna G Habashi kwa steji ili aje amtambulishe mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba
Captain Gadna G Habashi kwa steji akimtambulisha mama mzazi wa Kanumba
Na hii ni picha kubwa aliyopewa mama yenye sura ya Kanumba kama kumbukumbu yao iliyotolewa na gazeti hilo la BaabKubwa
DYNA akimpa msanii wa kike mkongwe Lady Jay Dee tuzo ya msanii bora wa kike
Yusuph Mlela alipanda jukwaani kuja kutoa tuzo ya mwigizaji bora wa kike katika tasnia hii ya filamu zetu za hapa bongo, na aliyekuja kuchukua tuzo hiyo ni Monalisa
Monalisa akiwashukuru BaabKubwa na mashabiki wake kwa ujumla
Madee alikuja kutoa tuzo ya mwimbaji bora wa kiume ambaye alikuwa ni Prof Jay na niliitwa mbele kuchukuwa tuzo hiyo kwa niaba yake kwamaana alikuwa hayupo Prof Jay
Producer Lamar alikuja kwa steji kutoa tuzo ya Producer bora wa mziki hapa bongo na aliyekuja kuchukuwa tuzo hiyo ni GOD FATHER WA BONGO FLEVA P.Funk Majani
Bob Junior huwa haniangushagi katika show zake,
Big Up sana Rich Mavoko unafanya poa sana katika show zako ila punguza mwili kidogo kwa maana nilikuwa nakutizama nikaona kabisa umeongezeka so hapo mbele kama panataka kutuna hivi.
Mr Blue kwa steji akimuita mkongwe mwingine kwenye bongo fleva Q.Chief waje waimbe wote
Q.Chief
BASI SAWA....Mambo ya binadamu hayooo
No comments:
Post a Comment