Pages
▼
CHELSEA WAMTIMUA ROBERTO DI MATTEO: GUARDIOLA, BENITEZ, REDKNAPP KURITHI MIKOBA
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoka katika menejimenti ya klabu hiyo Bodi ya timu ya Chelsea imechukua uamuzi huo baada ya maendeleo ya timu hiyo kwa siku za hivi karibuni kuonekana kutoridhisha na hivyo imeamua kumfuta kazi kocha huyo ili kuleta mabadiliko katika timu hiyo ili ipate matokeo na mwenendo mzuri.
Ingawaje kocha Di Mateo alikuwa bado anafanya vizuri katika mechi za ligi na kombe la FA na pia kuwa kocha aliyepata mafanikio mazuri katika Kombe la Klabu Bingwa La Ulaya msimu uliopita.
Mmiliki pamoja na bodi ya timu wameona timu imekosa mwenendo mzuri hivyo wameona ni bora kubadilisha meneja ambaye atachukua jukumu la kufanya timu ifuzu hatua ya mtoano katika mashindano hayo ya Klabu Bingwa La Ulaya na pia katika kuliwania taji la ligi kuu ya Uingereza (Barclays English Premier League.
Bodi hiyo ya timu ya Chelsea imemshukuru kocha Roberto Di Matteo kwa mchango wake mzuri wa kuijenga timu toka alipoichukua mpaka hapo alipofika nayo.
Bado haijaulikana ni kocha gani anayetarajiwa kuchukua mikoba ya kocha huyo lakini aliyewahi kuwa Kocha wa timu ya Liverpool Rafa Bennitez anatajwa na watu wengi kuwa ndiye anaweza kumrithi Muitaliano huyo. We unafikiaje..tupe chaguo lako.
No comments:
Post a Comment