SWALI
Mimi ni mama nimeolewa miaka 14 iliyopita. Nimezaa watoto wanne. Tatizo langu kubwa ni mume wangu ambaye ameyageuza maisha yangu kuwa jehanam. Kifupi ni mtu mkorofi, mhuni na asiyejali maisha ya familia, haishi kuniumiza. Hadi hapa nilipo kanikimbia mimi na watoto na anaishi na mwanamke mwingine. Nifanyeje.
JIBU
Maisha yana kanuni moja kubwa nayo ni kutodumu kwa vitu. (Labda milima ambayo sijaona ikitoweka ingawa nayo inatajwa kutoweka) Unayoyaona leo kesho unaweza usiyaone kesho na kila linapoondoka moja jingine huja. Ukilia leo kesho utacheka, ukifurahi utahuzunika, ukipata utakosa, ukitajirika utafirisika pia.
Hayo ndiyo maisha ya kila siku ya mwanadamu. Sasa ili uishi kwa raha kila ulipatalo sema litapita. Pambana na kila hali bila kuumizwa na kukata tamaa. Hayo yanayokusibu yatapita unachotakiwa kufanya ni kuishi wewe kama wewe na kutomtazama mumeo kama mkombozi wako.
Kwa kuwa kakukimbia washirikishe ndugu zake na wako wajue hilo, ili suluhu itafuwe ikishindikana jitume kutafuta maisha yako naamini utafanikiwa na utamudu kuwalea watoto wako. Siku za furaha yako zinakuja na mumeo atatambua kosa lake bila shaka.
Na wewe kama mdau wa ujanatz unalipi la kumshauri ?
No comments:
Post a Comment