Pages

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):



1. Kutokwa na damu
sehemu za siri

Dalili kubwa za miscarriage

ni mama mjamzito kutokwa

na damu (nzito au nyepesi)

sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi

hutoka kama zile zitokazo

mwanamke anapokuwa

kwenye siku zake na

huambatana na maumivu

makali ya tumbo chini ya kitovu.


2. Maumivu makali ya

viungo Dalili nyingine za mimba

inayotaka kuchoropoka ni

maumivu makali ya

mgongo, kiuno, nyonga na

tumbo chini ya kitovu.

Maumivu haya huanza taratibu lakini huongezeka

kadiri muda unavyozidi

kusonga mbele. Pia

huambatana na kutokwa

na damu kama ilivyoelewa

hapo juu.


3. Kutokwa na uchafu

sehemu za siri

Dalili nyingine kubwa ya

Miscarriage ni mama

mjamzito kuanza kutokwa

na uchafu wenye rangi sambamba na mabonge ya

damu sehemu za siri.


ANGALIZO: Dalili hizi pekee

hazitoshi kuashiria kuwa

tayari ujauzito umeharibika

ila mama mjamzito

anapoona moja kati ya dalili

hizi au zote, anashauriwa kuwahi hospitali kuonana

na daktari haraka

iwezekanavyo. Endapo mama atachelewa,

atakuwa anajisababishia

matatizo zaidi kwani sumu

za kiumbe kilichoharibika

huharibu mfuko wa uzazi

na kusababisha matatizo makubwa siku za mbeleni

ikiwemo ugumba.

No comments:

Post a Comment