Snoop Lion (dogg
Rapper mkongwe aliyejulikana kwa jina la Snoop Dogg kabla hajabadilisha na kuwa Snoop Lion, mwaka huu baada ya kuhamia kwenye muziki wa reggae na kulazimika kuchill Jamaica ili kukamilisha project yake ya album ya reggae, ameamua kujiunga na jamii ya Jamaica pia katika kusaidia kusolve tatizo la ukosefu wa chakula na matunda hasa kwa watoto.
Snoop Lion ametangaza kuwa na ushirika na Reed’s Ginger Brew ili kusaidia mradi unaoitwa Mind Gardens Project.
Project yake hii ambayo haipo kwa ajili ya kuingiza faida (non profit) , ina lengo la kuhakikisha inatengeneza bustani endelevu za jamii. Bustani hizo zitatoa matunda ya asili na mboga kwa ajili ya watoto nchini Jamaica.
Snoop mwenyewe aliandika statement, “nilipoenda Jamaica, tulichukua muda kwenda kutembelea hizi jamii huko Kingston, na niliadhiriwa sana na umasikini na ukosefu wa chakula bora kwa watoto.”
Snoop aliendelea kudondosha maandishi kwa feeling za alichokiona na kutoa ahadi, “hakuna mtoto atakaepata njaa. Baada ya inspiration niliyoipata kutoka Jamaica, najisikia msukumo wa kuchukua jukumu kutengeneza kitu ili kuirudishia jamii.”
Project hii imeshaanza tayari huko Kingston na imeshazifaidisha jamii mbili kubwa , Trench Town na Tivoli Gardens.
No comments:
Post a Comment