Joseph Mkanda (pichani) amekumbana na tatizo la dawa hizo
BAADHI ya wanaume wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa za kurefusha maisha wamejikuta wakivimba matiti yao na kuwa makubwa kama ya wanawake.
Joseph Mkanda (43) amekumbana na tatizo la dawa hizo ikiwa ni pamoja na kuvimba matiti. Mwanzoni alihisi ni kutopata chakula bora, lakini akagundua kwamba ni aina za dawa anazotumia.
“Naona aibu sana kutoka nje ya nyumba yangu, kwani nimepata matiti kama mwanamke…. Naona watu wakiniona watanicheka,” anasema mwananchi huyo ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Mtwara.
Mwingine huyu hapa!
“Nilipokwenda zahanati ya kijijini nikaambiwa hilo ni jambo la kawaida kwa watu walioathirika na Ukimwi, hivyo sijui la kufanya wala pa kwenda,” anasema Mkanda.
Mwanamke Salima Omar (36) mwenye watoto saba kutoka Mtwara anasema mwili wake umekumbwa na matatizo kibao tangu aanze kutumia dawa hizo. Mmoja wa watoto wake wa kike alifariki mwaka ......muda mfupi tu baada ya kuzaliwa kwake.
Hata hivyo, Salima ambaye ni mke wa Hassan, na ambaye mwili wake umejaa vipele, na maumivu sehemu mbalimbali za mwili, anaamini hali hiyo inatokana na kutopata lishe bora.
“Madawa haya ni makali mno, usipokula vizuri ni lazima yataivuruga afya yako,” anasema na kuongeza kwamba kuna siku analazimika kuyatumia madawa hayo bila kula chochote hususan anapokuwa mgonjwa sana.

Mwanamke huyo anasema kuna wakati hayatumii madawa hayo kutokana na ukosefu wa fedha ya chakula, kwani mumewe ni fundi wa baiskeli na yeye (Salima) hupoteza fedha anazopata kwa kunywea pombe. Hali hiyo imemsababishia kuuza mbuzi wote wa familia yake ili kumudu maisha.
Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka ......, Salima naye yuko katika mkumbo huo.
Kama zilivyo familia nyingi katika Wilaya ya Mtwara ambazo zinakabiliwa na upungufu wa chakula tangu mwaka ......, Salima naye yuko katika mkumbo huo.
Vilevile, licha ya kuwa mwathirika, mwanamke huyo bado anaendelea kuzaa. Miezi mitatu iliyopita alizaa mapacha ambapo mmoja wao alifariki na mwingine hali yake ni mbaya.Hata hivyo, wataalam wa tiba wamewashauri wanandoa hao kuacha kuzaa, jambo ambalo huenda wakakubaliana nalo.
No comments:
Post a Comment