KOMEDIAN aliyejitosa katika muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amefunguka kuwa hakuna kitu kigumu kama kuishi kisharobaro kwani kunahitaji gharama kubwa.
Akizungumza na ‘kachala’ wa Wikienda Staa Shopping aliponaswa hivi karibuni akifanya manunuzi ya nguo katika duka la Robby One lililopo Kinondoni jijini alisema ili uwe sharobaro wa ukweli inabidi usiwe mbahili katika kununua nguo kila mara ili uendane na staili hiyo ya usharobaro.
“Kweli kabisa ndugu yangu hutakiwi kuwa mbahili kwani ukiwa na tabia hiyo wavimba macho mitaani watakutungia jina la sharobaro mchafu,” alisema Sharo Milionea.
Komedian huyo alifanya shopping ya kununua vitu dukani hapo iliyogharimu kiasi cha shilingi laki mbili na ushee.
No comments:
Post a Comment