Flaviana Matata mlimbwende wa mitindo anayetangaza jina la Tanzania nchini Marekani akiwa na maskani yake kwenye jiji lisilolala, New York akipata picha alipokuwa akifuatilia mitindo nite 3 iliyofanyikia Capitol Heights, Maryland.
Flaviana Matata katika picha ya pamoja na mtayarishaji wa mitindo nite 3 Ma Winny Casey (kati) pamoja na mlimbwende Mtanzania Maggie Munthali atakaeiwakilisha Tanzania Usa kumtafuta Miss Afrika USA itakayofanyika Jumamosi hii kwenye ukumbi huo wa Hampton uliopo 207 W Hampton Place, Capitol Heights, MD.
Mratibu wa Miss Afrika USA akielezea jambo huku akisifia vazi la khanga.
Juu na chini nni mwana muziki wa Bonga Flava a.k.a malikia wa Zouk, Hafsa Kazinja akilishambulia jukwaa alipofanya show akishirikiana na Bendi ya Super Bakulutu yenye wanamuziki wa DRC waliotamba enzi hizo na wanaoendela kutamba Marekani kwa sasa akina Lokassa ya Mbongo, Gouma Lokito na kundi lake.
Lokassa ya Mbongo (kushoto) katika picha ya pamoja na mwanamuziki mwenzake ambae alishawahi kupiga na kundi la Koffi.
Wadau waliohudhuria onyesho hili la mitindo nite 3 wakipata picha ya pamoja.
Starlisha (wapili toka kulia) katika picha ya pamoja na wadau wa DMV, kutoka shoto ni Nick, Santa na kulia ni John Sitta.
No comments:
Post a Comment