AMBWENE YESSAYA 'AY'
Mbali na kudumu kwenye gemu la muziki kwa muda mrefu bado anaendelea kushika kasi kwenye anga za muziki huku akiendelea kufanya vyema kwenye upande wa Afrika Mashariki kwa kuweza kujinyakulia tuzo za channel o ya video bora ya mwaka 2012
Singel yake ya 'I don't wanna be alone' ndio iliyompaisha mpaka kujinyakulia tuzo hiyo, huku msanii huyo akiendelea kufanya vyema kwa kuteuliwa kuwa balozi wa kampuni ya simu za mikononi Airtel pamoja na kujitoa kwa jamii ikiwa ni moja ya mchango wake kwa jamii inayomzunguka na kusapoti kazi zake
Utafiti unaonyesha kuwa AY ndiye msanii anayeongoza kufanya kazi na wasanii wengi wanaowika kiuliwengu kwenye tasnia ya muziki, huku nyimbo zake zikiwa zinatikisa kwenye vyombo vya habari vya nje ikiwemo channe O
Video yake iitwayo 'Party Zone' ikiwa imeonekana kumpandisha zaidi kwa kuweza kupigwa mara kwa mara Channel O
Tangu ajikite kwenye gemu hilo (AY) amejikuta akifanya juhudi binafsi ili kuhakikisha anaufikisha muziki wake katika anga za kimataifa sambamba na kuupaisha kiujumla muziki wa bongo fleva kuendelea kutambulika zaidi kimataifa
Mbali na mafanikio hayo pia AY amekuwa ni miongoni wa wamiliki wa kipindi cha mkasi ambacho kinatoa fulsa kwa wasanii na wadau wa sanaa mbalimbali kuelezea mafanikio yao na mipango yao ya muziki kiujumla, hii ni moja ya mchango wa AY kwa jamii inayomzunguka
Wadau mbalimbali katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya wanatalajia kuwa 2013 kuendelea kuyaona mafanikio zaidi ya nyota huyo yatakayosababisha muziki wa bongo fleva kuzidi kustawi kwani muziki huu umekuwa ukitoa ajira kwa vijana.
ILUNGA KHALIFA 'CPWAA'
Japo kuwa hakutwaa tuzo za Channel O, nyota ya Cpwaa ambaye anajiita 'The King of Bongo Crunk' imezidi kuyafikia mafanikio mengine ambapo jina lake limekuwa jina tajwa kwenye tuzo hizo kwa kupitia single yake ya 'Hhmm' kwenye kipengele cha video bora ya mwaka 2012
Nyota huyo amekuwa na mafanikio mengi katika tasnia ya muziki kwa kuwa ni msanii wa pekee kuanzisha stairi ya kipekee iitwayo 'Crunk' hali ambayo imemsababishia kujizolea umaarufu mkubwa hususani kwa wanafunzi wa sekondary, pamoja na elimu ya juu.
Pasipo kuisahau singo yake nyingine iitwayo 'Action' inayofanya vizuri katika kumbi mbalimbali za disko akiwa amewashirikisha Ms Trinity, Ngwair na Dully Sykes ambayo pia ilitwaa tunzo za Kilimanjaro Music Awards 2012.
NASEEB ABDUL 'DIAMOND'
Nyota huyo ameonekan kufanya makamuzi ya kutisha kwa kutoa ngoma zake ambazo zimeendelea kuwa na mvuto kwa wadau na mashabiki kwenye tasnia ya muziki nchini na ndiye msanii
aliyeweza kupagawisha mashabiki wake hali iliyoenda sambamba na kupamba kurasa za
mbele za magazeti nchini.
Kutoka na kuipua ngoma zenye ubora wa hali ya juu anakuwa ni msanii aliyevunja rekodi
kwa kufanya shoo alizolipwa kwa gharama ya beijuu zaidi ya wasanii wengine kutoka
kwenye shoo zilizo andaliwa na mapromota.
Msanii huyo ambaye amevunja rekodi na kuleta mapinduzi katika tasnia ya muziki wa bongo fleva , baada ya kufanya onyesho yake iliyoitwa ‘Diamond’s are Forever’, kwenye Ukumbi wa Mlimani City, ambapo katika shoo hiyo aliifanya mwenyewe na kiingilio kikiwa Sh 50,000 jambo ambalo halijawahi kufanyika katika ulimwengu wa muziki nchini.
Nyota ya msanii huyo ilizidi kung'ara pale alipojibebea tuzo tatu za kilimanjaro music awards 2012, ikiwemo video bora ya muziki ya mwaka kwa kupitia nyimbo ya moyo wangu, tuzo ya mtunzi bora wa mwaka kwa kupitia singo ya mawazo, na kujibebea tuzo ya mtumbuizaji bora wa kiume wa mwaka huku akiwabwaga wasanii wengine kama Ally Kiba, Bob Junior, H. Baba na Mzee Yusup
Nyota huyo bado anaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia hiyo ya muziki na kuonekana kutoa ajira kwa baadhi ya vijana wa kitanzania kwa hatua yake ya kufanya usahili na kuwalipa wale watakaotumika kuonekana katika video ya wimbo wake unaojulikana 'nataka kulewa' ambao unafanya vizuri katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka
PAUL MATTHYSSE 'P FUNK'
Producer mwenye mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki wa bongo fleva kwa kuinua na kuibua vipaji vingi vya wasanii wa muziki huo vilivopata kufanya kweli na kumletea heshima aliyonayo hadi sasa katika muziki huo
Ameonyesha moja ya harakati zake zingine kukuza muziki huo baada ya hivi karibuni kufufua kundi lililokuwa limeanzishwa miaka 18 iliyopita linaloitwa 'No name' kwa kuwaongeza maproducer wengine watatu wakiwemo Dunga, Lamar, John Mahundi pamoja na Karabani ambaye ndiye aliyeanzisha naye kundi hilo
Kurejea upya kwa kundi hilo huku kukiwa na vichwa kibao vya maproducer nchini ni moja ya harakati za maprodyuza hao kuhakikisha muziki wa bongo fleva kufika katika ngazi ya kimataifa pamoja na kufanya vizuri katika soko lla muziki wa kimataifa kwa kuwa wao ni wataalamu wa kutengeneza muziki huo
'Hands Up' ndiyo single walioiachia ya kufunga mwaka huku wakiwa wanaandaa kazi nyingine ambazo zitakuwa katika santuri moja nyimbo zenye radha tofauti tofauti Afro Pop, Ragga, Bongo Fleva, Tradition wakiwa na lengo la kuuza ndani na nje ya Afrika
BEN POL
Msanii anayekuja kwa kasi na kupata umaarufu kwa haraka kupitia tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya anayefanya miondoko ya R&B huku akiwa amejizolea umaarufu kwa kuzimiwa na mademu wengi kitendo kilichomsababisha kuitwa 'Sukari ya mademu'
Nyota yake ilizidi kung'ara pale alipojinjyakulia tuzo ya wimbo bora wa RnB – My number 1 fan katika kinyaganyiro hicho alifanikiwa kuwabwaga nyota wengine wa muziki wa bongo fleva Belle 9 na 'Nilipe Nisepe', Hemed na 'Usiniache', pamoja na msanii Jux.
Uimbaji wa stail yake umeonekana kuvuta hisia kwa waimbaji chipukizi wengine kupata kugeza uimbaji huo na kujikuta wanapata mafanikio kupitia nyimbo zake mfano mshindi wa Bongo Epiq Star Seach 2012 Waltery
Amezidi kupata mafanikio mwaka huu kwa ngoma zake kufanya vizuri hali iliyomfanya kuteka mashabiki wake huku nyimbo ya Pete ikionyesha kumtambulisha vilivyo kwenye gemu ya muziki kwa mwaka huu
OMMY DIMPOZ
Msanii aliyejizolea umaarufu kwa muda mfupi huku akiwa na singo moja iliyomtambulisha kwenye gemu na kusababisha kunyakuwa tuzo za Kilimanjaro Muic Awards kwenye kipengele cha msanii bora anayechipukia , kwa kupitia wimbo wake wa Nai nai aliomshirikisha Ally Kiba, ambapo aliwabwaga Darasa na wimbo wa Darasa, Rachel kupitia wimbo wa Kizunguzungu, Abdul Kiba na wimbo wa 'Sio demu' na Beatrice kwa wimbo wa Nabisha
Nyota huyo ameweza kufanya vizuri kwa kipindi chote cha mwaka huu huku akiwa amefyatua ngoma nyingine inayokwenda kwa jina la 'Baadaye' ikiwa sambamba na video yake ambapo sasa ameweza kuwateka vyema mashabiki wake
RECHO
Msanii chipukizi ambaye ameweza kuteka mashabiki wa muziki huo kwa ufundi wake wa kuimba na kucheza pamoja na kuweza kumiliki jukwaa kwa umakini wa hali ya juu, huku akiwa anatamba na nyimbo ya 'Upepo' pamoja na single ya Nashukuru umerudi
Mwanadada huyo mwenye sauti ya ndege mnaa aliyejizoelea umaarufu kutokana na staili yake kufanana na mwanadada aliyemkuta kwenye gemu mwenye miondoko kama hiyo hiyo Ray C
BARNABA
Msanii huyo nyota yake ilianza kungara pale alipotoka na ngoma yake iliyokwenda kwa jina la 'Milele daima' na aliweza kujinyakulia tuzo ya muimbaji bora wa kiume wa mwaka huu zilizotolewa na Kilimanajaro Music Awards
Kwa kipindi cha mwaka huu chote msanii huyo aliendelea kufanya vizuri kwa kutoa nyimbo ambazo zimempatia mafanikio kwa kuweza kufanya shoo kubwa sehemu mbalimbali, utafiti unaonyesha kuwa nyimbo ya Magumegume imeonekana ikipendwa sana na mashabiki pamona na wadau wa muziki huo kwa kile kilichoimbwa kuendana na mazingira halisi ya watazania
Nyota huyo bado anaendelea kufanya vizuri kwa kuwa mbunifu kenye kazi zake na kubadilisha staili tofauti tofauti zikiwemo aina ya mavazi anayovaa pamoja na mitindo ya nywele hali hiyo inamsababisha kubadilika na kuwa na mvuto wa tofauti kwenye kazi zake
Barnaba amezidi kujiongezea mafanikio kwa kujenga familia huku akiwa amejaliwa kupata mtoto wa kiume ikiwa ni moja ya mafanikio aliyoyapata kwa mwaka huu
ROMA MKATOLIKI
Msanii aliyeibuka kwenye gemu ya Hip Hop na kuonekana kuwa na kipaji kikali katika aina ya muziki huo na kuweza kufanya vyema huku akiwa amewateka mashabiki wengi, hali iliyosababisha kufanya vema kwenye shoo zote alizoonekana kwenye jukwaa moja na wasanii wengine wa miondoko ya kizazi kipya
Mathematics ndio singo ambayo imeonekana kuteka mashabiki wengi na kumpa 'mashavu' lukuki kwenye shoo zilizoandaliwa na mapromota mbalimbali
Roma ambaye nyota yake imezidi kungara pale alipojinyakulia tuzo mbili ya msanii bora wa Hip Hop na wimbo bora wa Hip Hop kwa mwaka huu tuzo zilizoandaliwa na Kilimanjaro Music Awards, huku akionyesha uwezo wa hali ya juu kwa kuwabwaga wakongwe wa muziki huo
SHETTA
Msanii huyu ameweza kuvuna mafanikio kwa haraka mwaka huu kwa kushirikisha wasanii mahili katika kazi zake ambapo singo yake iliyoenda kwa jina la 'Nidanganye danganye'aliweza kumshirikisha msanii mahili Diamond na kuweza kumpaisha kufanya vyema katika tasnia ya muziki
Baada ya kutamba kwa ngoma hiyo aliibuka tena na ngoma ya pili iliyoenda kwa jina la Bonge la bwana ambayo ndio ngoma aliyoiachia mwishoni mwa kufunga mwaka
Msanii huyo kupitia ngoma hiyo imemfanya kuendelea kuwa gumzo hali inayomuezesha kupata 'mashavu' katika mitoko ya kugonga shoo mbalimbali, mbali na hayo msanii huyo amezidi kupata mafanikio kwa kuweza kuzindua (websity) yake ambayo itamsaidia kujitangaza na kutangaza muziki wake kwenye ngazi ya kimataifa
Mbali na hayo Shetta amejaliwa kupata mke na mtoto ambayo ni moja ya mafanikio ya haraka katika hatua yake ya muziki kwa mwaka huu
Hao ni baadhi ya wasanii ambao wameonekana kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwa mwaka huu
No comments:
Post a Comment