Ni mada iliyoonekana kuwagusa wengi na huenda ni kutokana na ukweli kwamba, matukio ya baba kufumaniwa akifanya dhambi na hausigeli wake yamekuwa yakishamiri sana huko mtaani.
Wapo walionipigia simu na kuniambia si kwa wanaume tu bali kuna wake za watu nao wamekuwa wakifanya mapenzi na ‘mashamba boy’ wao, hilo nalo tutalizungumzia siku zijazo ila kwa leo tumalizie kwanza yale ambayo huwafanya waume za watu kutembea na mahausigeli wao.
Kama uko sambamba na mimi utakumbuka niliishia pale ambapo niliwataja mahausigeli mcharuko. Wapo mabiniti ambao walianza kujihusisha na vitendo vya ngono tangu walipokuwa wadogo.
Kuna ambao walipitia biashara ya uchangudoa na baada ya kushindwa huko wakaingia mtaani na kuanza kutafuta kazi za ndani.
Ukijichanganya na ukakutana na kabinti kazuri ambako kalipitia uchangudoa na ukaamua kukaajiri kama kahausigeli kako, mambo hayawezi kuwa sawa. Mumeo atategwa na mwisho atashawishiwa kukusaliti.
Sasa inaingiaje akilini mke kuridhia kumuajiri ‘hausigeli’ ambaye kwa macho tu anaonekana hajatulia? Unamuajiri hausigei ambaye siku ya kwanza tu anataka umpe sehemu ya mshahara wake akafanye ‘shopping’ halafu unakubali, unajitaka kweli?
Hujiulizi ana sababu gani ya kununua lotion, pafyumu na nguo tena za kimitego wakati ndiyo kwanza anaanza kazi? Anataka ampendezee nani kama siyo kumtega mumeo?
Kimsingi kuna hawa wafanyakazi ambao ukikubali wawe wasaidizi wako ndani ya nyumba watakusaidia hadi ‘kumhudumia’ mumeo. Kikubwa ni kuangalia yupi ana vigezo vya kuwa hausigeli wako na yupi hafai.
Mke kutojali
Kuna wanawake wengine naweza kusema hawajali, yaani hata wakiona dalili za wazi kwamba wanachukuliwa waume zao, wanachukulia poa tu. Hivi utakuwa ni mke makini kweli kama utamruhusu hausigeli wako akae akiangalia TV sebuleni na mumeo wewe ukiwa chumbani umelala?
Ni sahihi kweli mke kusafiri na kumuacha mumewe na hausigeli, wawili tu ndani ya nyumba ambayo si ya kupanga? Je, ni sahihi mume kwenda ‘out’ na hausigeli huku mke akibaki nyumbani?
Kwa mke makini hawezi kukubaliana na mazingira hayo lakini kama hujui wapo wanawake wa ajabu ambao wala hawaoni hatari kuwaachia waume zao kuwa na ukaribu huo na wafanyakazi wao wa ndani. Sasa katika mazingira hayo unatarajia nini?
Wanaume ambao hawajatulia
Kuna waume za watu wengine wamekuwa na tamaa za kijinga sana kiasi cha kufikia kuwashawishi mahausigeli wao wawape penzi. Hili limekuwa ni tatizo kubwa na kimsingi mke anapobaini kuwa mumewe anamsumbua mfanyakazi wao, hatua za haraka zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment