Harakati za wanawake zimeshika hatamu siyo barani Afrika tu hata kwingineko duniani kote na imekuwa kama jambo lisilotakiwa kuchukuliwa katika hali chini. Harakati zake zimeanzia mbali zimesafiri kutoka katika safari ambapo wanawake kutaka kufanya mambo sawa na wanaume na kuhakikisha na kuona ndoto zao zinakuwa katika maisha yao. Maazimio tofauti yamefikiwa ikiwemo lile maarufu la mkutano wa Beijing ambalo lililenga katika kuwapa nguvu wanawake kuhakikisha wanakuwa na nguvu katika masuala ya uchumi, jamii, siasa na utamaduni. Leo kuzunguka zaidi ya nchi 50 za Afrika, kuna hisia hizo miongoni mwa wanawake kwamba ndoto zao zinakuwa kweli. Siku hizi ni ngumu sana kumuona mwanamke wa kiafrika akifanya jambo bila mtazamo huo katika shughuli zake. Mafanikio ya uwiano ni mkubwa sana kwamba wanawake 10 kati ya 11 ni wanaongoza makampuni makubwa au wanasimamia miradi yao. Jambo muhimu ni sababu kwamba mafanikio ambayo yamepatikana ni mazao ya wasichana, wazima na wacheshi, ambao wamepiga hatua kutoka kutokuwa na kitu hadi kimiliki kitu. Na jambo kubwa kwa wanawake hawa kuwa mafanikio yao yanapelekea kuiamsha jamii kuwa na mtazamo chanya. Orodha hii inaangalia wanawake wa kiafrika 20 ambao ni wadogo kiumri na wana nguvu ambao wametajwa na jarida la Forbes. Wanawake hao wana umri chini ya miaka 45 ambao kwa namna moja ama nyingine wanaliweka bara la Afrika katika hali haki, usawa na amani.
Yolanda Cuba – South Africa
Ni mmoja kati ya wanawake wenye msimamo na wanaoheshimika nchini Afrika Kusini, Yolanda Cuba anafaa kupigiwa mfano kama wanawake viongozi katika makampuni duniani. Hapo mwanzo alikuwa tayari kutengeneza jina yeye mwenyewe wakati ambao wanawake wengine hawakujua kitu gani cha kufanya katika maisha yao.
Mwanafunzi huyo wa zamani katika Chuo Kikuu cha Cape Town na Kwazulu Natal, Yolanda alikuja kuwa kiongozi mdogo zaidi nchini Afrika Kusini wakati akiliongoza kundi la Mvelaphanda, JSE kampuni ambayo imesajiliwa katika kipindi akiwa na miaka 20. Yolanda ameendelea kung’ara na kuwa mfano wa kuigwa na vijana wa kiAfrica. Yolanda, ambaye ni mjumbe wa kamati ya Uwekezaji na Wakfu ya Taasisi ya Nelson Mandela, amehudumu na anaendelea kuhudumu makampuni mengi nchini Afrika K usini kama vile SAB Limited, Reunert Limited, Steinhoff International Holdings, Absa Group Limited na Health Strategic Investment Limited.
Funmi Iyanda – Nigeria
Alipozaliwa alipewa jina la Olufunmilola Aduke Iyanda. Ni mjumbe wa Taasisi ya Uobgozi Africa pia ni mjumbe Taasisi ya ASPEN Institute’s African Leadership Initiative. Funmi ni moja ya waandishi wa habari maarufu nchini Nigeria. Ni CEO wa Ignite Media. Iyanda ana umri wa miaka 41 na amepata kila kitu katika masuala ya uandishi wa habari nchini Nigeria na anaendela kupata zaidi.
Anaongoza program ya jarida maarufu ya Talk with Funmi, ambayo inahusu maisha ya kila siku nchini Nigeria, ambayo inawahusisha wasanii mbalimbali, waandishi, celebrities na wanasiasa na watu mbalimbali kutoka jamii ya wanigeria. Anaonekana kuwa na nguvu nchini Nigeria, na ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa na wenye kufanya maamuzi. Mapenzi yake na television yameanza baada ya kutayarisha na kutangaza kipindi kiitwacho “Good Morning Nigeria”. Kwa miaka mingi sasa ya utangazaji wa television, uandishi wa makala na kuhudumi blog, Funmi daima amekuwa akitoa hisia na uelekeo wake kwa vijana wa Nigeria.
Elsie S. Kanza – Tanzania
Hivi karibuni ametajwa na Baraza la Uchumi Duniani, World Economic Forum (WEF) kama kiongozi mdogo wa dunia, Kanza anaendelea kung’ara katika kila sehemu ya maisha yake. Kwa sasa ni Mkurugenzi, kiongozi wa Africa katika Baraza la Uchumi Duniani (WEF).
Kabla ya kujiunga na WEF, alikuwa katika serikali ya Tanzania akihudumu kama mshauri msaidizi wa uchumi.
Pia amefanya kazi na Central Bank of Tanzania. Kanza amewahi kufanya kazi katika Wizara ya Fedha kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, akihudumu nafasi ya Personal assistant. Anamiliki shahada za BSC katika usimamizi wa biashara ya kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani, Umahiri wa Sanaa katika Maendeleo ya Uchumi kutoka kituo cha Maendelo ya Uchumi, Williams College, U.S.A. huku akimiliki pia Cheti cha masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde MSC.
Magette Wade – Senegal
Wade amezaliwa nchini Senegal, ametumia miaka yake ya kwanza ya elimu nchini Ujerumani na Ufaransa lakini baadaye akajikuta yupo katika mitaa ya jiji la San Francisco nchini Marekani, ambako ya kuanzisha Adina World Beverages ilianzia. Mwaka 2011, jarida la Forbes lilimuorodhesha Wade kama mmoja wa wanawake wadogo wenye nguvu Africa.
Amependezwa na hadithi yenye mafanikio ya Silicon Valley start-ups, ambaya yalimuongoza kuzaliwa kwa Adina, Wade ameshuhudia ndoto zake zikiwa kweli. Sasa bidhaa za Adina World Beverages zinapatikana sehemu kubwa ya dunia hii. Anazungumza lugha ya utamaduni ya Wollof ya nchini kwake Senegal na lugha za Kiingereza na Kifaransa. Domo limeifanya kampuni yake kuwa na thamani ya dola za kimarekani 3.2 million. Wade anasema kuwa yuko mbioni kuanzisha kampuni nyingine, Tiossano, ambayo itakuwa inatengeneza bidhaa zenye mchanganyiko wa tamaduni tatu yaani Dakar, Paris, na San Francisco, sehemu ambazo amewahi kuishi.
Ory Okolloh – Kenya
Daima amekuwa anapigania mambo mazuri kwa wakenya, Okolloh amekuwa akifanya kampeni ya wazi dhidi ya serikali juu ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki huku akivutiwa na uchaguzi mkuu ujao. Ni mwanasheria. blogger na mwandishi. Okolloh ni muasisi mwenza wa myandao wa bunge ujulikanao kama Mzalendo mwaka 2006, kuongeza ufanisi wa serikali kwa lengo la kuhifadhi miswada, matamko, wabunge, na mambo mengineyo.
Mwaka huo huo wa 2006, akatambuliwa kuwa mmoja wa wanawake wenye ushawishi katika teknolojia. Mhitimu huyo wa Havard Law School, Okolloh, pia ni muasisi wa Ushahidi, anafanya kazi kama mshauri katika Taasisi moja isiyo ya Serikali na ana blog yake binafsi iitwayo KenyanPundit.
Bethlehem Tilahun Alemu – Ethiopia
Raia huyu wa Ethiopia mwaka uliopita alitajwa na kama kiongozi bora na Baraza la Uchumi Duniani, World Economic Forum. Akiwa mdogo alicheza katika mitaa ya jamii ya kimasikini ya Zenabwork, jijini Addis Ababa alikozaliwa, Alemu amekuwa shujaa katika biashara ya viatu. Rajamu yake ya SoleRebels, ambayo hivi karibuni itakuwa ya kwanza katika biashara huria ikipata leseni kutoka Oganizeshani ya Dunia ya Biashara Huria (WFTO), ni moja ya biashara ambayo imefanikiwa kutoka nchini Ethiopia.
Kwa sasa, viatu vya Alemu vinauzwa katika nchini 55, nyingi zikizwa kwa rejareja, nani anamsaidia mwanamama huyu kukifanya kile alichokifikiri kuwa kweli? Ana umri wa miaka 32 lakini tayari ameajiri watu 75 wa muda ote na zaidi wa vibarua 200 ambao wanafanya kazi ya kusamabaza. Mwaka huu jarida la Forbes limemuorodhesha kama Mwanamke wa Afrika aliyenikiwa zaidi.
Dambisa Moyo – Zambia
Anaheshimika kwa kupinga kwake misaada kutoka nje kwa Africa, Moyo ni mmoja ya wasemaji wakuu wa bara la Afrika katika masuala ya mikingamo na masuala yanayotakiwa kuangaliwa kwa makini. Ametajwa na Time Magazine kama mmoja katika watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani.
Kazi za Moyo mara nyingi huonekana katika machapisho kama vile Financial Times na Wall Street Journal. Ana Shahada ya Uzamili katika Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Oxford na Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Harvard. Moyo, ambaye anaingia katika Bodi ya Rajamu maarufu, amepata Shahada ya Awali katika Chemistry na MBA ya masuala ya fedha kutoka American University jijini Washington D.C.
Saran Kaba Jones – Liberia
Jones ni muasisi wa FACE Africa, taasisi ambayo inajishughulisha na masuala ya kutoa misaada kwa wasiojiweza kama maji safi na salama kwa watu waishio vijijini nchini mwake Liberia. Maelfu wa watu wa Liberia wananufaika na project yake. Hadithi ya Jones inahusiana kwa karibu na watoto wengine wa Liberia. Baada ya kuondoka nchini Liberia kabla ya kile kilichojulikana kama vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 14, amejea nyumbani mwaka 2008 kuweka mambo sawa na mazuri kwa watu ambao aliwaacha wakati anaelekea nchini Marekani.
Kazi mradi yake ya kwanza ilikuwa mjini Barnersville, iliwekwa katika jamii ya watu 600 nchini Liberia. Ikifanya kazi kwa kushirikiana na oganizesheni nyingine, FACE Africa imesaidia kuweka pampu za mikono na kujenga pampu za chini. Kwa sasa mradi wa Barnersville unasambaza maji safi na salama kwa kunywewa na binadamu lita 20,000 kila siku katika mamia ya makazi ya watu nchini Liberia.
Juliet Ehimuan – Nigeria
Mwaka 2011, kwa wingi ilizungumziwa kuhusu matangazo ambapo kampuni ya Google ilipomtaja kama meneja wa nchi. Akisimamia kile kinachojulikana kama kampuni kubwa ya masuala ya mtandao barani Africa; Ehimuan anaiwakilisha kampuni ya Google katika level hiyo pia kufanya miradi ya kuendeleza biashara yake na nafasi za ushirika. Weledi wake katika masuala ya teknolojia inashibiri masoko ya dunia, hasa bara Ulaya, Mashariki ya Kati, (EMEA) Africa na Marekani. Ameanza shughuli zake katika kampuni ya mafuta inayojulikana kama Shell Petroleum Development Company akihudumu nafasi Performance Monitoring na msimamizi wa uhakiki wa ubora, na amehudumu kama meneja mipango katika kampuni ya Microsoft UK kwa miaka sita, na managing Strategic Projects katika kampuni ya MSN EMEA. Baadaye alikuja kuwa meneja wa mchakato wa biashara katika kampuni ya MSN Global Sales na Marketing Organization.
Ameachana na kampuni ya Microsoft mwaka 2005 na kuanza kazi katika SI Consulting Ltd UK, akitoa huduma ambayo iliwaunganisha viongozi wa biashara barani Africa na ulimwengu mwingine. Ehimuan ana elimu ya MBA kutoka London Business School, shahada ya Uhandisi wa Kompyuta kutoka Chuo Kkikuu cha Obafemi Awolowo, Ile-Ife, na Post Graduate katika masuala ya Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Cambridge, UK.
Khanyi Ndhlomo – South Africa
Waweza kumwita mpanzi wa Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini; Ndhlomo amejitengezea jina mwenyewe. Mmiliki wa Ndalo Media, inayochapisha Destiny Magazine na Destiny Man. Kabla ya kuanzisha kampuni ya Ndalo, amehudumu kama mhariri katika True Love Magazine kwa miaka 8.
Mwaka 2003, alitajwa na Media Magazine kama mwanamke mwenye ushawishi katika vyombo vya habari nchini Afrika Kusini. Mafanikio yake yamechagizwa baada ya kuweka historia ya kuwa mtu mweusi wa kwanza kusoma taarifa ya habari katika televisheni ya SABC wakati huo akiwa na umri wa miaka 20.
Julie Gichuru – Kenya
Anaonekana kama sura ya televisheni ya Kenya, Gichuru anaonekana mara mbili akiwa kama nanga na akiwa kama mtendaji wa Citizen TV, ambayo ni maarufu sana nchini Kenya. Ni mwanachama wa kuaminika wa African Leadership Initiative, ambayo ni sehemu ya Young Global Leaders wa Baraza la Uchumi la Dunia.
Amewahi kupata tuzo ya Martin Luther King, amehudhuria project kadhaa za UNICEF, mtandao wa Aspen Global Leadership na Africa Global Leadership.
Chimamanda Adichie – Nigeria
Ni mmoja kati ya waandishi walio na mafanikio barani Africa, akifanya juhudi za ndani na nje kuhakikisha kuwa anaisimamisha fasihi ya Africa. Akiwa na umri wa miaka 45, anaendelea kufanya vizuri katika taaluma yake. Mwaka 2006, riwaya yake ya pili ya Half of a Yellow Sun, ilishinda zawadi ya Orange mwaka 2007. Riwaya yake ya kwanza, Purple Hibiscus, imetolewa mwaka 2003 ilipata tuzo ya Jumuia ya Madola kama Kitabu bora cha kwanza mwaka 2005.
The Thing Around Your Neck, ni kitabu chake cha tatu ambacho ni mkusanyiko wa hadithi kimechapishwa mwaka 2009. Mwaka 2010 aliorodheshwa miongoni mwa The New Yorkers “20 under 40” masuala ya ubunilizi; na hadithi yake ya “Ceiling”, iliwekwa katika mkusanyiko wa 2011 ulioitwa The Best American Short Stories.
Olga Kimani-Arara – Kenya
Huyu ni msemaji wa kampuni ya Google nchini Kenya ambapo katika nchi ya nyumbani kwake, Kenya, anaheshimika kutokana na kuishi kikawaida hasa katika sekta ambayo alikuwa anafanya kazi kabla. Mwaka 2012 aliachana na kampuni ya Google kwa lengo la kufanya mambo mengine.
Kabla ya kujiunga na kampuni ya Google, alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Safaricom. Microsoft Certified System Engineer, Kimani-Arara anamiliki Shahada ya Umahiri ya Uhandisi wa Usimamizi wa biashara kutoka shule ya biashara ya Manchester. Pia ana shahada ya Electrical and Electronics Engineering.
Phuti Malabie – South Africa
CEO wa kampuni inayomilikiwa na kuendeshwa na mtu mweuzi ya Shanduka Group of South Africa, Malabie aliorodheshwa mwaka 2008 na Wall Street Journal kama mmoja kati ya wanawake 50 duniani wanaopaswa kutupiwa macho. Mwaka 2007, Baraza la Uchumi la Dunia lilimchagua kuwa Global Young Leader, katika orodha ambayo iliwajumuisha pia wanawake wadogo walio piga hatua katika maendeleo duniani.
Kabla ya kujiunga na Shanduka Group, Malabie, mwenye umri wa miaka 41, alikuwa kiongozi wa Project Finance South Africa unit katika Benki ya Maendeleo Kusini mwa Africa. Mwaka 2009, alipewa tuzo ya Mwanamke mwenye Ushawishi mkubwa katika Serikali na Biashara, tuzo ambayo ilitolewa na Financial Services. Pia alikuwa makamu wa rais wa Fieldstone kuanzia mwaka 1997 hadi 2003.
Isis Nyongo - Kenya
Nyongo ni makamu wa rais na mkurugenzi mtendaji wa mtandao huru mkubwa duniani wa simu na matangazo ya mtandao wa InMobi.
Anafanya kazi katika MTV, mtandao wa kazi unaoongoza nchini Kenya wa MyJobsEye, na Google. Ni muhitimu wa Harvard na Standford.
Ndidi Nwuneli – Nigeria
Mwasisi wa LEAP AFRICA, taasisi ambayo inajihusisha na utoaji wa elimu na mafunzo ambayo lengo lake ni kuwaandaa viongozi bora wa kiafrika hapo baadaye. Nwuneli ni miongoni mwa wajasiriamali wa Nigeria ambao wamefanikiwa sana.
Ni kurugenzi mtandaji mwasisi wa taasisi ya FATE, ambayo inajihusiha na masuala ya ujasiriamali na maendeleo miongoni mwa vijana wa Nigerian, amepewa heshima na tuzo kadhaa ikiwemo moja aliyopewa na Baraza la Uchumi la Dunia huko Davos mwaka 2003 na tuzo ya Uhodari kutoka Klabu ya Biashara Afrika katika shule ya biashara ya Harvard mwaka 2007.
Stella Kilonzo – Kenya
Kilonzo hivi karibuni alikuwa ni mtendaji wa Capital Markets Authority, Kenya.
Baada ya miaka minne na nusu ya kuishi kwa muda nchini Marekani, Kilonzo alirejea nchini Kenya na kufanya kazi Pricewaterhouse Coopers, akiwa kama mshirika mkuu katika idara ya Corporate Finance Advisory Services.
Jonitha Gugu Msibi – South Africa
Msibi anaendesha maisha kupitia Ernst & Young akisifika kwa uongozi wake imara, amevuna mengi kutoka miongoni mwa njia zake.
Anachukuliwa kuwa ni mmoja wa wanawake wanaoheshika zaidi nchini Afrika Kusini miongoni mwa wanawake waliofanikiwa.
June Arunga – Kenya
Arunga ni mwasisi na mtendaji wa kampuni ya Open Quest Media LLC, ambayo iko New York.
Anahudumu pia katika Bodi ya taasisi ya Moving Picture na Global Envision kama mwanachama, na anafuata International Policy Network (London, UK), pia na Istituto Bruno Leoni (Milan, Italy).
Lisa Kropman – South Africa
Kabla hajakuwa katika shughuli zake, Kropman alihidumu kama Mshiriki katika Werksmans Attorneys. Kwa sasa, ni mwasisi wa kundi la biashara ambayo inalenga kuwainua watu iliyopo katika miji ya Johannesburg, Alexandra, Soweto, Cape Town, Philippi, King Williamstown na Botswana, Swaziland na Rustenburg.
The Business Place, kama ambavyo inajulikana na Waafrika kusini wengi inalenga kuwatia matumaini wafanya biashara wapya. Tangu mwaka 1997, amehudumu nafsi kadhaa katika kampuni ya Investec Limited ikiwepo ya uongozi wa juu, Employment Equity Forum; Head, Corporate Social Investment Division; na Catalyst katika kundi la CIDA City Campus. Anamiliki shahada ya awali katika Sayansi ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town na shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand.
No comments:
Post a Comment