Pages

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA


Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo. 

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani. 

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma. 


Viongozi waandamizi wa CHADEMA wamesema, kutiwa mbaroni Godbless Lema ni mkakati wa CCM wa kukabiliana na nguvu ya chama hicho kikuu cha upinzani ambayo imeteka jimbo la Arusha mjini.

 Salum Bendera amezungumza na Bw. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye anaanza kuelezea jinsi chama chao kilivyopokea hatua ya kutiwa mbaroni Mbunge Godbless Lema.

No comments:

Post a Comment