Jamaa Achomwa Kisu cha Kifuani na Demu Baada ya Kumlazimisha Kufanya Nae Mapenzi Kwa Lazima na Kutaka Kumbaka
Onyinyechi Orakwuelum alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akitimiza umri wa miaka 18. Hata hivyo siku hiyo ambayo huwa ni ya furaha miongoni mwa binadamu wengi, imegeuka na kuwa ya majonzi na matatizo baada ya mwanadada huyo kuwa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Kijana ajulikanaye kwa jina la Ayobami, ambaye binti huyo anadai alidhamiria kumbaka na katika kujitetea kwake alifanikiwa kumpiga kisu na kujisalimisha mwenyeweSiku ya tukio Ayobami alimpigia simu binti huyo na binti akamwambia ya kwamba yupo nyumbani na ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, jamaa akamuuliza kama alikuwa na mipango yoyote ya sherehe, binti akamwambia hapana ni mapumziko na kuikumbuka tu siku hiyo, Ayobami akamwambia wakutani mida ya saa 1 jioni maeno fulani, binti alikubali, na alipoeenda wakaenda mpaka nyumbani kwa Ayobami ambaye alitumia muda mfupi kukaa katika laptop yake na baadae akamfuata na kumwambia ya kwamba anampenda na anaomba awe mpenzi wake. Onyinye alikataa sababu alihisi ni utani lakini jamaa alivyozidi kumsogelea karibu, binti huyo akagundua kuwa Ayobami amelewa, naye akakazania kupewa japo penzi kwa siku husika ikiwa hatamkubalia basi angemfanyia kitu mbaya.
Baada ya kukuru kakara za muda mrefu, jamaa akaelekea jikoni na kuchukua kisu ambacho alikuwa akimtishia msichana huyo huku akianza kumvua nguo kwa nguvu, kwa bahati kisu hicho kilidondoka chini na ndipo Onyinye alikiokota na kumchoma nacho, akaskia sauti kutoka kwa Ayobami akilalama kwamba kamchoma, Onyinye alikimbia na kwenda kutoa taarifa kituoni, polisi walipofika eneo la tukio walimkuta jamaa kashafariki na kisu kilimuingia katika moyo.
Mpaka sas binti huyo anashikiliwa na polisi mpaka uchunguzi utakavyo kamilika.
No comments:
Post a Comment