Pages

TAMASHA LA KILI MUSIC AWARDS NDANI YA UWANJA WA JAMHURI DODOMA.....OMMY DIMPOZ APIGWA CHUPA NA MASHABIKI JUKWAANI..!!

Ommy dimpoz arushiwa chupa na mawe jukwaaani dodoma na kushindwa kufanya show ya kilimanjaro muzik award dodoma. Wadau wa dom wasema kamwe msanii yoyote atakaye mdisi msanii wa dodoma awatamkubari kufanya show dom na watamshusha jukwaani kama walivyo fanya leo
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.

 Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
 Msanii wa Hip hop Mwenye tuzo nne za Kilimanjaro Tanzania Music Awards  2013,Kala Jeremier akifanya vitu vyake usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
 Mashabiki hawakutaka kabisa kupitwa na taswira za show hii.
 Ni shangwe kwa kwenda mbele ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi sasa.

No comments:

Post a Comment