MARIAM KHAMIS 'PAKA MAPEPE' KUZIKWA KESHO MAGOMENI - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » MARIAM KHAMIS 'PAKA MAPEPE' KUZIKWA KESHO MAGOMENI

MARIAM KHAMIS 'PAKA MAPEPE' KUZIKWA KESHO MAGOMENI


DAR ES SALAAM, Tanzania
MAZISHI ya aliyekuwa mwimbaji mahiri wa taarabu wa nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’, yanatarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Magomeni Makuti wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mariam (pichani) ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa TOT Taarab, alimefariki alfajiri ya kuamkia leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kifo chake kikitokana na matatizo ya uzazi, ingawa mtoto wake yu salama.
Kwa mujibu wa Baba Mdogo wa marehemu anayetajwa kwa jina moja la Sembuli, alisema kuwa, wamefikia uamuzi wa kumzika marehemu kesho, baada ya kuombwa na Mkurugenzi wa TOT Kapten Komba kufanya hivyo ili wapate kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.
Kundi la taarabu la TOT, liko mjini Dodoma kwa hivi sasa kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo msiba wa marehemu huko nyumbani kwa baba yake mkubwa Magomeni Makuti, Mtaa wa Ndovu Bar, yanakotarajiwa kufanyika mazishi hayo.
Mariam Khamis alitamba sana na wimbo wa Mapaka Mapepe alouimba akiwa na Melody, kiasi cha kumpa jina hilo la utani, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, kisha Five Stars na hatimae TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ulikuwa ni ‘Sidhuriki na Lawama’ ambao unatamba sana hadi sasa anapopchukuliwa na mauti yaliyoelezwa kutokana na Kifafa cha Uzazi alichokumbana nacho baada ya kujifungua kwa operesheni kubwa.
Wasanii mbalimbali wa muziki nchini, hususani wa Taarabu, wameelezea kustushwa na kifo cha Mariam, ambapo Habari Mseto ulishuhudia waimbaji na mashabiki mbalimbali kwenye Hospitali ya Muhimbili, ulikohifadhiwa mwili wa marehemu.
Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template