UDAKUSPECIALLY;NYUMBA NDOGO IMEATHIRIKA MIE MZIMA - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » UDAKUSPECIALLY;NYUMBA NDOGO IMEATHIRIKA MIE MZIMA

UDAKUSPECIALLY;NYUMBA NDOGO IMEATHIRIKA MIE MZIMA

Habari
mi ni kijana mwenye mke na mtoto mmoja, nina mpz nje ya ndoa yangu ambaye anakaa kwao. nimekuwa na uhusiano nae kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili sasa; sijawahi kwenda nae kupima licha ya yeye kudai mara ya mwisho alipima mwaka 2007 na alikuwa safi lakini mimi huwa napima mara kwa mara.
hivi karibuni alikuwa mbali nami kwa masomo ingawa mawasiliano yalikuwepo kama kawaida na nilikuwa namtania kuwa hata kama naibiwa basi tumieni kondom, utani huo ulionekana kumkera hata kufikia kusema akiridi kabla ya kukutana tupime kwanza nikamkubalia.
amerudi na jana tukaenda kupima alikuwa ananipigia mara kwa mara kuniuliza tunaenda saa ngapi?

tulipofika eneo la tukio kama kawaida tulipewa ushauri nasaa na kuulizwa maswali kama kwa nin mriamua kuonana kimwili kabla ya kupimwa binafsi nilijibu kutokana na afya yake niliamini hana maambukizi (ni binti mnzuri kwa muonekano, hips za kuvutia na ---- lakutosha ni raha hata kuongozana nae) na yeye alisema aliniamini.

tukatolewa damu ingawa ilikuwa tofauti kidogo na nivyowahi kupima kabla, kabla walikuwa wanatoa damu kidoleni kama wanavyopima malaria ila sasa walinitoa hapo wanapotoa damu kama unataka kumuongezea damu mtu.

baada ya muda tuliitwa kupewa majibu na mambo yalikuwa hivi
baada ya maneno ya daktari aliendelea kutuuliza maswali kama itaonekana mwenzako ameathirika (nilimtambulisha kama mke wangu) utafanyaje nikajibu nitaendelea kuwa nae na nitatumia kondomu kwake ila yeye alijibu ana uhakika yupo vizuri; mi nikadakia nakumwambia usimchagulie docta jibu.
baadae daktari akaniambia nipo vizuri nakumwambia mwenzangu samahani kwa majibu hayo nitakoyokupa vipimo vinaonesha umeathirika. sikuamini na bado siamini
daktari alienda mbali zaidi kwa kutuonesha kuwa baada ya kumpima kwa kipimo cha kwanza akampima kwa mara ya pili, tatu na baadae akaamua kubadilisha kipimo akatumie kingine (alituonesha) lakini majibu bado ni yale yale.
Mapokea ya majibu ya mwenzangu
hakushtuka sana kitu kilichonishangaza alianza kulia baada ya dk 20 kupita
haamini matokeo ana taka kurudia kupima, aliendelea na kulia huku majuto ya kiwa kwa kiasi kidogo ila alikuwa mara kwa mara akiomba nisimuache na mimi nirimhaidi kuto muacha.
nilitumia muda mwingi kumnyamazisha ingawa hakutulia kwa asilimia mia, na baadae nilimpeleka kwao ambapo wazazi wake walikuwa wameondoka na yeye alibaki na wadogo zake, tulipofika kwao aliendelea kulia waliniuliza analia nini nikawajibu tumekorofishana lkn namwambia yameisha hataki kuelewa akawa anajibu kuwa mi mwongo na alitaka kusema ukweli nikamkataza na mara akawasha simu yake akitaka kumpigia simu mamake nikamnyang'anya.
alikuwa na kadi ya harusi ya mamake aliniambia ataenda kwenye sherehe na baadae alienda (mambo haya yote yalianza saa kumi na mbili jioni) alikuwa huko nilikuwa namfuatilia kwa kumpigia simu alikuwa haoneshi kuwa na wasi wasi sana ila aliomba nisimuache, na asubuhi ya leo ameenda kunisani kama kawaida.

Ninachohisi
Aidha alikuwa anajua ameathirika au alikuwa anajua ametembea na mtu aliyeathirika hivyo alikuwa na uhakika wa zaidi ya asilimia 50 kuwa ameathirika kwa sababu.

  1. Alitaka kumlazimisha daktari kutoa majibu kama haja athirika (rule out the doctor)
  2. hakupokea majibu kwa mshtuko sana.
  3. anaomba kuto achana na mimi badala ya kufikiria zaidi kuathirika kwake
  4. ameweza kwenda kwenye sherehe ya harusi just after an hour (nilipenda aende kwa ajili ya kupoteza mawazo) lakini sikutegemea akubali au iwe rahisi kwake
  5. ameweza kwenda kanisani leo


Nataka
  1. Nimpeleke hospitali nyingine akapime tena na hata kama majibu yataendelea kuwa kama yalivyo sasa basi apewe ushauri nasaha ili aondokane na mawazo ya kuathirika ni mwisho wa maisha na kuwa huru kimawazo.
  2. niendelee kuwa nae karibu kwa muda fulani then nitampotezea (ushauri unahitajika kutoka kwako msomaji)


Naomba ushauri kuhusu hali hiyo ikiwemo uhusiano wetu wa kimapenz.i ili kumuondoa mawazo nilimwambia nitaendelea kufanya mapenzi nae ila kwa kondomu sio kama ilipokuwa kuwa awali ambapo kondomu ilikuwa haitumiki.

ndigu zangu ukimwi upo tuwe makini na wapenzi wetu tusipime kwa macho huyo ambaye namzungumzia ukimwona alivyoshiba huwezi amini kuwa ameathirika.

naomba kama huna cha kuchangia pita tu utani singefurahia sana
Share this article :

3 comments :

  1. Mambo mengi yansababisha mtu kuwa positive. Angalia kwenye entenet ' Houes of numbers. Katika vipimo vyao wakiona kuna antibodies basi wanachukulia kwamba una vvu. Antibodies ndinvyo vinaweza kuonekana lakini virusi havijawahikuonekana katika vipimo vyao. Antibodies hutokea katika mwili ili kupambana na kitu kinachoingia katika mfumo wa damu. Muulize mkeo kama alitumia antibiotic nyingi pia husababisha positive. H.I.v ipo lakini bado kuna watu wanaingizwa kwenye kundi hilo kimakosa . Kwahiyo tahadhari inatakiwa hapo pengine no kweli ana hiv. Chunguza kwanza kabla ya kuanza dawa ikiwa sfya yake ni nzuri.

    ReplyDelete
  2. we kwa nini usibaki na mkeo,achananae huyo,mchepuko sio dili kaa na mkeo

    ReplyDelete
  3. Kwanza niseme pole sana ndungu yangu kwa yote ayo yaliokupata.
    Husiachane na dada huyo ili kumusaidia zaidi saikolojia yake.
    Ila tu uwe makini kwakila jambo asante.
    N.B: na mimi nimesha wahi kutana na swala kama hilo licha ya kwamba tunazidiana tabaka!

    ReplyDelete

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template